Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Kim Simplis Barrow, Mke wa Waziri Mkuu wa Belize na Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Wanawake na Watoto. Mama Barrow kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa ndio walioandaa mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi kuzungumzia masuala ya kuwawezesha wanawake na wasichana kifedha.na “First Ladies Global Call to Action Conference on Women and Girls’ Financial Health.” Tarehe 25 Septemba,2014.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Joyce Banda, Rais Mstaafu wa Malawi muda mfupi kabla ya kuanza mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi ulizungumzia namna ya kuwawezesha wanawake na wasichana kifedha huko New York tarehe 25.9.2014. 
Joyce Banda (ex-president wa Malawi)alishindwa kwenye uchaguzi wa mwisho....unawezaje kumwita mstaafu? Hivi mfano mfanyakazi akiondolewa kazini kwa sababu zozote halali utamwita mstaafu? Huyu aliutaka u-prezidaa, kura hazikutosha you see....how do you call her retired president?
ReplyDelete....ni vizuri kuweka kumbukumbu sawa: huyu ni "Madam Joyce Banda aliyewahi kuwa rais wa Malawi na kushindwa kutetea kiti chake katika unchaguzi uliomwingiza madarakani...."