Mkurugenzi mtendaji wa Statoil Hulge Lund (Kushoto) akitumia moja ya kompyuta za maabara itakayotumika kuendeleza vijana wa Mtwara katika shindano la Mashujaa wa Kesho linaloendeshwa na Statoil. Kulia ni Katibu tawala wa Mkoa wa Mtwara Bw. Alfred Luanda na katikati ni mmoja wa wanafunzi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa shindano hilo.
Baadhi ya vijana waliohudhulia hafla hiyo katika Maabara ya komputa zilizounganishwa katika mtandao wa intanet, komputa hizo zitatumika kuwafundisha vijana namna ya kuendeleza mawazo ya biashara kuwa Mpango wa Biashara.
Katibu tawala wa Mtwara Alfred Luanda akikata utepe kuashiria ufunguzi wa maabara ya komputa itakayotumika kuwaelimisha vijana wa Mtwara katika shindano la biashara la Mashujaa wa Kesho, Wanaoshuhudia ni Mkuu wa chuo cha Stalla Maris Mchungaji Dr Longino Rutagwerera Kamuhabwa na Mkurugenzi mtendaji wa Statoil Helge Lund.
Picha No.5.
Msanii wa bongo fleva akitumbuiza katika hafla ya ufunguzi wa shindano la biashara la Statoil “Mashujaa wa Kesho” iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Stella Maris huko Mtwara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...