Mabondia Said Kasimu wa Amana kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hamad Mbonde wa Magereza wakati wa mashindano ya kutafuta kumi bora ya kila uzito kwa mabondia jijini Dar es salaa yanayoandaliwa na chama cha ngumi za Ridhaa mkoa wa Dar, DABA Kassimu alishinda kwa point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Hamad Mbonde wa Magereza kushoto akipiga ngumi bila matumaini yoyoyo na mwenzake Said Kassimu  wa Amana akimpiga konde la kulia wakati wa mashindano ya kumi bora yanayoendesha na chama cha ngumi za ridhaa mkoa wa Dar es salaam kila jumamosi katika ukumbi wa Manyara Park Tandale CCM Manzese 
Bondia Said Kassimu wa Amana akinyooshwa mkono juu kuashilia ushindi
Mabondia Shabani Mohamed wa JKT kushoto akipambana vikali na Uwesu Hamadi wa Temeke wakati wa mashindano ya kumi bora ngumi za RIdhaa yanayoandaliwa na chama cha ngumi mkoa wa Dar es salaam na kufanyika kila jumamosi katika ukumbi wa Manyara Park CCM Tandale Manzese Dar es salaam Mohamed Alishinda kwa point mchezo huo picha na Super D. 
---------------------------------------------------------------------------------
MASHINDANO ya ngumi kupata mabondia 10 bora wa  mkoa wa Dar es salaam yanayoendeshwa na chama cha ngumi za ridhaa 'DABA' yameendelea kushika kasi kwa wiki ya pili sasa. Mashindano hayo yanayofanyika kila jumamosi katika ukumbi wa Manyara park CCM Tandale Manzese jijini Dar es salaam yamekuwa yakiibua vijana mbalimbali wenye vipaji vya mchezo wa masumbwi nchini kutoka kila kona ya jiji la Dar es salaam
Akizungumzia mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Mwenyekiti wa 'DABA' Akaloli Godfrey amesema mashindano hayo yatakuwa yakiendelea kila wiki mpaka wafikie mabondia wote wa dar wapo katika viwango vya ubora nchini na kuwataka watu binafsi makampuni na taasisi za kiserekali kusaidia mashindano hayo yanayoenderea kutimua vumbi kila wiki ambapo inakusanya vijana wengi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...