OKTOBA
12 mwaka huu katika kuadhimisha siku ya amani duniani viongozi wa dini
wanatarajia kujitupa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na
kulisakata kabumbu safi kabisa, wakiwa na lengo la kudumisha amani
iliyopo nchini.
Mtanange
huo utawajumisha Masheikh,Maimamu,Maaskofu,Wachungaji na Mapadre na
mgeni rasmi katika mchezo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
ambaye tayari amekubali kuungana na viongozi hao wa dini.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam leo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ndiye
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mchezo huo alisema kuwa Mkuu wa
Mkoa huo, Said Sadick atakuwa mwamuzi msaidizi akisaidiwa na Kamishna wa
Kanda Maalumu, Seleman Kova na Afande IGP Ernest Mangu atakuwa mpuliza
kipyenga wa kati.
Alifafanua
kuwa viongozi hao wa dini tayari wameshaanza mazoezi kwa jili ya
kujiweka tayari kwa ajili ya kufanya vizuri katika mtangane huo wa
kuhamasisha amani na ulivu nchini katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume
jijini Dar es Salaam.
Aliongeza
kuwa wanaendelea na mazoezi hayo chini ya kocha mjerumani na Serikali
ya Mkoa wa Dar es Salaam, itazipeleka timu mbili mkoani Morogoro kwa
ajili ya kujifua zaidi na mtanage huo utakaokuwa wa kukata na shoka
kutokana na jinsi timu za viongozi hao wa dini zilivyojipanga kucheza
mchezo huo wa amani.
Ili
kujindaa vema na mchezo huo Mwakilishi Mkazi wa Shirilka la
KAS,Tanzania, Stefan Reith, alikabidhi kwa Sheikh wa Dar es Salaam,
Alhad Salum vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo mipira, jeshi na viatu.
Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salim (katikati),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
kuhusu maandalizi ya mchezo wa kirafiki wa mpira wa miguu kati ya
Masheikh na Mapadre utakaofanyika uwanja wa Taifa Octoba 12-2014. Alhadi
Salim ndiye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi wa mchezo huo.
Kushoto ni Katibu wa Kamati ya Amani kutoka Kanisa la Anglikana Padri
John Solomon na Mwakilishi Mkazi wa Shirilka la KAS,Tanzania Stefan
Reith.

Mwakilishi Mkazi wa Shirilka la KAS,Tanzania Stefan Reith (kushoto), akimkabidhi baadhi ya vifaa vya michezo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salim kwa ajili ya maandalizi wa mechi hiyo. HABARI/PICHA NA PHILEMON SOLOMON
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...