Kamishina Mkuu Msaidizi Programu ya Vijana wa Chama cha Skauti Tanzania (TSA), Mary Anyitike (kushoto), akimvisha Nishani ya Skauta, Safi Shabani kiongozi wa Skauti kutoka Shule ya Sekondari Lugoba iliyopo Bagamoyo mkoa wa Pwani wakati wa hafla ya kufunga mashindano hayo jana.
Kamishina Mkuu Msaidizi wa Utawara Bora wa Chama cha Skauti Tanzania (TSA), Mwalimu mstaafu John Lusunike (kushoto), akikagua skauti kabla ya kuanza mashindano Septemba 23,2014.
Vijana wa Skauti wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa tayari kwa ukaguzi.
Vijana wa Skauti wa Kikosi cha Simba kutoka Mkoa wa Morogoro ambao walikuwa washindi wa Mashindano ya Skauti katika nchi za Afrika Mashariki yaliyofanyika nchini Burundi mwaka 2013 wakiwa tayari kwa ukaguzi huo kabla ya mashindano hayo yenye lengo la kuwapata washiriki katika mashindano ya Afrika Mashariki yatakayofanyika nchini Rwanda Desemba 2014.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...