Pichani ni sehemu mojawapo ya mitaa ya Musoma mjini ikiwa na muonekano wa watu wachache mara baada ya kunaswa na Camera ya Globu ya Jamii mapema leo mchana,mji huo umegubikwa na simanzi na manjonzi makubwa kufuatia ajali mbaya ya mabasi mawili yaliyogongana uso kwa uso likiwe gari ndogo,na kupelekea kuondoa uhai wa watu takribani 40 na zaidi katika kijiji cha Sabasaba wilayani Butiama mkoani Mara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Natoa pole sana kwa watu wote walohusika kwenye ajali hii mbaya. Natoa pole kwa watu wote walioondokewa na wapendwa wao. Natoa pole sana kwa Watanzania wote.
    Haya ni matokeo ya uendeshaji mbaya ambao chanzo chake ni mfumo mzima unaoendesha usalama barabarani. Madereva wengi wamejenga jeuri ya kutoheshimu sheria na kanuni za usalama barabarani kutokana na ushwahiba kati yao na askari. Hivi kweli kuna dereva wa mabasi ambaye hajawahi kumhonga askari wa usalama barabarani?
    Taarifa zisizorasmi, zinaonyesha kuwa kila dereva wa gari kubwa, hutoa hongo mara mbili kwa wiki. Hizi ni taarifa nilizopewa na ndugu zangu wanaojishughulisha na biashara ya usafiri. Rushwa za mara kwa mara zipo pia Mamlaka ya Mapato ambapo, magari yaliyomengi yanaendeshwa bila kulipa ushuru au kodi inayostahili. Hii ni pale mwenye gari anapokubali kuwapa nusu ya kodi jamaa wa TRA.
    Ncchi nyingine kama Marekani, mianya ya rushwa imeondolewa kwa kutumia technologia.
    Askari anapomsimamisha dereva, mazungumzo kati yao hurushwa moja kwa moja kwenye kituo Traffic Management Centre, na kurekodiwa, na hufuatiliwa na Afisa mkuu.
    Hapa kwetu, ni tofauti kabisa. Utazushiwa jambo wakati wa kuhojiana na usipoonyesha kuwa tayari kutoa rushwa, utapelekwa kituoni.
    Hivi tuisaidieje serikali kukabiliana na matendo haya maovu?
    Ndugu zetu wanazidi kuteketea kwa ajali kuliko hata magonjwa mengine.

    ReplyDelete
  2. Hivi watanzania tuna vuchwa vigimu kiasi gani?

    Kama hatuelewi ya darasani, ya vitendo na mfano je? Kweli madereva wa mabasi na magari makubwa hawaoni ajalinza wengine? hawasikii maafa yanayotokea kila kukicha? au ni ujasiri gani huu jamani?

    Hii lami sasa badala ya kuleta maendelea imegeuka kuwa balaa la kupunguza uhai wa watanzania.
    Kweli tuma laaniwa...

    ReplyDelete
  3. Wafiwa poleni sana. Tunawaombea tu. Na tunasali haya maswala ya rushwa yatokomee. Kilio cha wengi husikilizwa na Mungu, hakika jibu lipo. Amani iwatangulieni wote.

    ReplyDelete
  4. Nafikiri haya ni matokeo ya kila mmoja wetu kutokuwajibika ipasavyo. Kila mtu anapaswa kuilaumu nafsi yake ndio amnyooshee kidole mwingine. Wadau wengi wana nyooshea kidole trafic, lakini jee madereva kwanini wafikie hapo pa kutoa rushwa??? Inamaana amevunja sheria! Abiria nao wanapokuwa katika vyombo hivi vya usafiri wawe na dhamana kamili na maisha yao. Nikiwa namnaaninisha pale ambapo unaona dereva anachukuwa dhamana ya maisha yako na kuyaweka rehani unapaswa kuchukua hatua. KIla mmiliki wa basi ahahakikishe anaweka namba za simu katika basi ambapo pale abiria akiona dereva anakiuka taratibu aweze kumjulisha mwenye gari. Pia namba za simu za maafisa wa polisi nazo ziwekwe katika mabasi kulingana na route ya hilo basi. Mwisho kwakweli trafiki mjue kuwa pasipo nyie kubadilika hizi ajali hazitakwisha. Nikitoa mfano wa hivi karibuni nilikuwa nikisafiri kati ya Dar Moro nikakutana na gari ambalo limebeba abnormal load likiwa linaendelea na safari yake wakati giza tororo limeshaingia na gari hili lilipita eneo ambalo trafik wapo na waliliruhusu kuendelea na safari. Sasa kama huyu dereva wa lori hajali uhai wake jee wale ambao wanahatarishiwa maisha nani awatete kama sio nyie??? Jamani tuwajibikeni tusimtupie Mungu lawama kila kukicha!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...