TUNAUNGANA NA WATANZANIA WOTE KATIKA KUOMBOLEZA MSIBA MKUBWA WA TAIFA
"Jana September 5 2014 kwenye eneo la Sabasaba Mjini Musoma ilitokea ajali mbaya sana ya mabasi mawili yakiwa na abiria na kulihusisha gari jingine dogo ambapo majeruhi ni zaidi ya 70 na waliofariki ni 39 Wanawake kwa Wanaume kwa mujibu wa taarifa mpya za vifo zilizotoka."
JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA IMEPOKEA TAARIFA ZA AJALI KWA MASIKITIKO  NA MSHITUKO MKUBWA SANA.
TUNAWAPA POLE NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WOTE WALIOPOTEZA WAPENZI WAO KATIKA AJALI HIYO,TUNATOA POLE KWA WATANZANIA WOTE NYUMBANI NA UGHAIBUNI KWA TUKIO  HILI LA KUSIKITISHA.  MWENYEZIMUNGU AWALAZE MAHALA PEMA PEPONI NDUGU ZETU, NA WALE AMBAO NI MAJERUHI MWENYEZIMUNGU AWAJAALIE NAFUU YA HARAKA NA WARUDI KATIKA SHUGHULI ZAO ZA KILA SIKU.
INASIKITISHA SANA KUONA AJALI KAMA HIZI ZA BARABARANI ZIMEKITHIRI SASA NA TAKWIMU YAKE NI KUBWA KWA MWAKA INATISHA. NI MATUMAINI YETU SOTE  ZITACHUKULIA HATUA KALI ZA KUDHIBITI HALI  HII YA KUTISHA NA KUSIKITISHA SANA.
TARATIBU ZIFUATWE ZA UKAGUZI WA VYOMBO VYA USAFIRI NA WAFANYAKAZI WOTE WA MAKAMPUNI YA USAFIRI.  MAKAMPUNI YENYEWE NAYO YAKAGULIWE KWAKINA SANA.
TUNAMPONGEZA MH WAZIRI MWAKYEMBE KWA HATUA ZA AWALI ALIZOCHUKUA KWANI SASA BASI WANANCHI HATUTAKI KUSIKIA AJALI HIZI ZA AJABU AMBAZO NYINGI ZINATOKEA KIZEMBE PASIPO NA UNGALIFU WA MADEREVA.
NA WATAKAO BAINIKA KUWA NA MAKOSA BASI WACHUKULIWE HATUA STAHIKI.
KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUOMBOLEZA YA  MSIBA HUU MKUBWA TUNAMUOMBA MUNGU ATUPE UVUMILIVU NA  UPENDO ZAIDI KWETU SOTE.

MUNGU IBARIKI AFRIKA
MUNGU IBARIKI TANZANIA


Kagutta N.Maulidi
Katibu mkuu
Jumuiya ya Watanzania Italia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...