Kamati ya Lugha na utamaduni, Jumuiya ya Watanzania Washington DC, Maryland na Virginia (DMV) inapenda kuwaalika wana DMV na wadau wote wa Lugha ya Kiswahili kwenye mkutano na viongozi wa Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) utakaofanyika siku ya Ijumaa Septemba 26, 2014 kuanzia saa nane mchana. Hii ni Fursa ya kukutana wa Wahadhiri wa lugha ya Kiswahili kutoka Vyuo mbali mbali hapa Marekani kwa lengo moja la kuendeleza lugha yetu ya Kiswahili. Anuani ya Ukumbi wa Mkutano vitafuata baadaye.
Songa mbele na Kiswahili.
Tunaomba wale mtakaoweza kuhudhuria kujiandikisha na kama unaswali pia wasiliana kupitia Mwanakamati na Kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania hapa DMV wafuatao hapo chini:
Mwanakamati Mkuu: Bi. Asha Nyang’anyi (301) 793-2833 
 Makamu Katibu ATC-DMV : Mhe. Bernadeta Kaiza 240-704-5899
                                            

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Endeleza kiswahili lugha inayounganisha Afrika mashariki na kati.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...