Kutoka kushoto ni Gwiji wa muziki wa dansi nchini Mzee Kassim Mapili akiwa amekaa kwenye kitanda cha hospitali ya Taifa Muhimbili  kushoto ni Rais wa Shirikisho la Muziki wa Dansi Tanzania Addo November alipokwenda kumjulia hali  leo asubuhi hospitalini hapo.

NA BONGOWEEKEND BLOGSPOT.COM
HALI ya mwanamuziki nguli Kassim Mapili aliyelazwa katika Hospitali  ya Taifa  Muhimbili katika kitengo cha moyo inaendelea vizuri imehafamika.
Mapili ambaye awali alilazwa katika Hopitali ya  Mwananyamala  kutokana na kusumbuliwa na  maradhi ya mapafu kujaa maji  pamoja na moyo kujaa maji ambako alilazwa kwa muda wa siku nne kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Muhimbili juzi  mchana.
Hayo yalisemwa leo na Rais wa Shirikisho la Muziki  Addo November  ambaye aliefika hospitalini hapo mapema asubuhi kumjulia hali Mapili  ambapo alikiri kuwa amelazwa katika wodi  namba moja  katika Taasisi ya Moyo baada ya kutolewa  katika wodi ya uangalizi maalumu (ICU), Muhimbili.
Aidha November ametoa rai kwa wadau na wanamuziki  viongozi  mbalimbali  kujitokeza kwa wingi kwenda kumjulia hali gwiji huyo wa muziki ikiwa ni sehemu ya kumpa faraja kwa ujumla.
 “Mzee wetu anaumwa sana na amevimba sana  miguu hivyo  ni wajibu wa kila mmoja wetu kutoa msaada wa hali na mali” alisema November.
Wakati Mapili akiwa amelazwa mama yake mzazi  aliyetajwa kwa jina la  Hajena Mussa  Mchikita amefariki usiku wa juzi nyumbani kwake Nachingwea  na atazikwa  leo mkoani Songea alisema November .

Mapili  alitamba na nyimbo za ‘Rangi ya Chungwa’, ‘Mayasa’ ambao aliuimba na Marehemu TX Moshi William enzi za uhai wake  na kutamba vilivyo katika miaka ya 1980.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mzee Kassim Mapili tunakuombea afya njema Mwenyezi Mungu akuvue ugonjwa huo na kukupa afya zaidi,wewe ni mmoja wa wakongwe adimu katika historia ya muziki wa dansi Tanzania.
    Tunakuombea Afya njema Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi upone kwa haraka baba.
    Wadau
    FFU-Ughaibuni
    www.ngoma-africa.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...