Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 24 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Mwigulu Nchemba akitoa hotuba yake wakati akifungua mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo Septemba 10 mpaka Septemba 12,2014.Katika hotuba yake hiyo,Mh. Nchemba wameutaka Mfuko wa PPF kuhakikisha wanapanua wigo kwa kuongeza wanachama wengi kutoka kwenye setka binafsi hasa wananchi wa kipato cha chini ikiwemo wajasiriamali.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI,ARUSHA.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF,Alhaj Ramadhan Khijja akitoa hotuba yake mapema leo asubuhi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 24 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio akizungumza leo kwenye Mkutano wa 24 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa PPF,unaofanyika leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.
Mgeni Rasmi katika Mkutano huo,Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,William Erio wakati wa Mkutano wa 24 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa PPF,unaofanyika leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha.
Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Titus Kamani (kushoto) akikabidhi Mfano wa Cheti,Muwakilishi wa Chama wa Wavuvi kutoka Ukerewe,Alphonce Mukama wakati wa Mkutano wa 24 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa PPF,unaofanyika leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,Jijini Arusha. Wapili kushoto ni Mgeni Rasmi katika Mkutano huo,Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Mwigulu Nchemba.
Picha ya pamoja na Baadhi ya Washindi wa tuzo mbali mbali za uchangiaji wa Mfuko wa PPF.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Huyu mwigulu hata tai bendera, kweli umekunywa maji ya bendera

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...