Mhandisi Edwin Nnunduma toka wakala wa amajengo Tanzania (TBA)akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa nyumba mbili zinajengwa katika kila mkoa kwa ajili ya makazi ya majaji wakati wa ziara ya waandishi hao iliyolenga kujionea hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo.
Moja ya jengo la kisasa lenye gorofa 4 lililopo Mbezi beach Dar es salam litakalopangishwa kwa watumishi wa Umma,jengo hilo liko katika hatua za mwisho kabla kuanza kupangishwa ili kupunguza tatizo la makazi kwa watumishi hao.
Mhandisi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Bw. Edwin Nnunduma akiwaongoza waandishi wa habari kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba zaidi ya 150 zinazojengwa katika eneo la Mabwe Pande Jijini Dar es salaam ambapo nyumba hizo zitauzwa kwa watumishi wa umma.
Mafundi wakiendelea na ujenzi katika mradi wa nyumba zaidi ya 150 zinazojengwa na TBA ambapo nyumba hizo zitauzwa kwa watumishi wa umma ikiwa ni moja ya mikakati ya Serikali katika kuondoa tatizo la makazi kwa watumishi hao.
Mhandisi Edwin Nnunduma toka wakala wa amajengo Tanzania (TBA) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu lengo la mradi wa nyumba zaidi ya 150 katika eneo la mabwe pande ambapo nyumba hizo zitauzwa kwa watumishi wa umma ikiwa ni sehemu ya mpango wa Serikali kupitia wakala huo kujenga nyumba 10,000.Picha na Frank Mvungi-Maelezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...