Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akimkabidhi zawadi Mwanamichezo aliyeiletea Wizara ushindi katika mashindano ya SHIMIWI na Meimosi mwaka jana Bibi. Niuka Chande. Mchezaji huyo aliibuka mshindi katika michezo ya Draft na kurusha Tufe na kuiletea Wizara vikombe viwili. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel na Mwenyekiti wa Timu ya Wizara Dkt. Margareth Mtaki.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwaaga wachezaji wa timu ya Wizara hiyo wanatarajia kwenda mjini Morogoro kesho kwa ajili ya mashindano ya SHIMIWI yatakayoanza kuanzia tarehe 27 septemba hadi Oktoba 11.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akiwa amenyanyua juu Kikombe cha ushindi wa kwanza kwa mchezo wa Draft katika mashindano ya SHIMIWI mwaka jana ambacho kilinyakuliwa na mchezaji watimu ya Wizara ya Habari Bibi. Niuka Chande (mwenye taki suti nyeusi)kushoto Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel akifurahia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...