Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama mbaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASAT) akizungumza katika tamasha
la Uimbaji na Uchangiaji wa Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea jijini Dar es Salaam na kuahidi
kutoa sh. milioni 6 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kanisa hilo. Msama
alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo akimwakilisha Waziri wa Habari
Vijana Utamaduni na Miochezo, Dk. Fenela Mukangala.
Mchungaji Emmanuel Masanja 'Masanja Mkandamizaji' aliguswa na kutoa ahadi ya shilingi milioni 1 katika hafla hiyo.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Tabata Matumbi, Mchungaji Christosiler Kalata akimkabidhi Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama sehemu ya mchango walioahidi
katika tamasha la Uimbaji na Uchangiaji wa Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Segerea jijini Dar es Salaam.
Usharika huo ulitoa ahadi ya sh. laki 7.
MJUMBE wa Baraza la Sanaa la
Taifa (Basata), Alex Msama ametoa kitita cha sh. mil 6 katika harambee
ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika
Segerea.
Msama ambaye alikuwa mgeni
rasmi katika hafla hiyo, alitoa kiasi hicho katika harambee hiyo ya kufanikisha
ujenzi huo, iliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubelee jijini Dar es Salaam,
huku akitoa na ushuhuda wa maisha yake mpaka kufikia hatua aliyofikia sasa.
Akizungumzia ushuhuda huo,
Msama aliwataka waumini kuiga mfano wake kwa kujitolea bila ya kugeuka nyuma,
kwani ana imani Mungu yupo na anatenda muujiza kama alioutenda kwake.
"Unajua mimi katika
maisha yangu hakuna ninayemwamini zaidi ya Bwana Yesu, kwa kuwa bila ya yeye
mie nisingekuwa hapa nilipo, kwa taarifa yenu wapendwa mimi nilishakuwa dereva
taxi, nilishakuwa kondakta wa daladala, lakini Mungu ni mwema na anatenda
muujiza mpaka mimi kuwa hivi," alisema Msama.
Msama ambaye ni Mkurugenzi wa
Kampuni ya Msama Promotions, aliongeza kuwa hata hivi karibuni katika ajali
aliyoipata akienda Dodoma licha ya kupinduka gari mara nne lakini alitoka akiwa
hai.
Harambee hiyo iliyoenda
sambamba na mnada, ilihudhuriwa na wasanii mbalimbali wa muziki wa Injili kama
Masanja Mkandamizaji, Edson Mwasabwite aliyeimba wimbo wa Ni kwa neema tu.
Mbali ya kiasi hicho
alichotoa, Msama pia alichangia katika mnada uliofanyika katika tamasha hilo na
kununua mtungi wa gesi kwa sh. laki 5.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...