Mmoja
wa Marappa mahiri kutoka nchini Marekani atambulikae kwa jina la
Clifford Joseph Harris,'T.I' ni mmoja
wa wanamuziki watakaoangusha bonge la shoo la kusambaza upendo kwa
wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake,katika onesho la Fiesta 2014
linalotarajiwa kufanyika ndani ya
Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam Oktoba 18.
T.I atafanya makamuzi pamoja na wasanii wengine mahiri wa hapa nchini,watakao pangwa kushusha bonge la burudani kwa wale watakaobahatika kupangwa kwenye orodha ya Oktoba 18, mwaka huu jijini Dar.
Nguli huyo mwenye albamu nane ambazo ni I'm Serious, Trap Muzik, Urban Legend, King, T.I. vs. T.I.P., Paper Trail, No Mercy na Trouble Man: Heavy Is the Head ambapo nyingi kati yake zimefanya vyema katika soko la muziki.
T.I ameshinda tuzo tatu za Grammy tangu aanze safari yake ya muziki.
Baadhi ya singo kali alizoachia mkali huyo na kufanya vyema ni "Bring Em Out", "What You Know", "Big Shit Poppin' (Do It)", "Swagga Like Us" (FT Kanye West, Jay-Z na Lil Wayne), "Dead and Gone" (FT Justin Timberlake), "Ball" (FT Lil Wayne) na "No Mediocre" (FT Iggy Azalea).

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...