Watu wawili Wanadaiwa kupoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa vibaya kufuatia ajali mbaya iliyotokea leo  katika  eneo la  Sanangula nje kidogo ya mji wa Songea mkoani Ruvuma,ikilihusisha basi la Super Feo linalofanya safari zake kati ya Songea - Makambako lililoacha njia na kugonga mti. Aidha inaelezewa kuwa chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa ni mwendo kasi.
 Sehemu ya basi hilo la Super Feo lionekanavyo pichani likiwa limepondeka pondeka baada ya kuacha njia na kugonga mti
Baadhi ya Wasomalia wema wakiwasaidia majeruhi waliopatwa na ajali ya basi hilo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ee kweli Tanzania nimeamini kuna jinamizi la ajali. Mbona naiogopa Tanzania sasa kama sio nchi yangu? Ee Mungu tunakwenda wapi, jamani tumrudie Mungu nafikiri Mungu kachukia kwa uhuru tuliopewa na tunautumia vibaya. Mungu utusamehe dhambi zetu. Da!

    ReplyDelete
  2. Mambo gani haya jamani mbona ajali zinatishia maisha.

    ReplyDelete
  3. Hivi mbona mgari yana pondeka vibaya hivi? Hili linazua swala la usalaama wa vyombo vyetu. Ndiyo kusema mabasi haya ni kama mabati au ? Mimi nashangaa sana kuona mabasi yanayoishia kupondeka hivi. Mbona ajali kama hizi nchi nyingine tena Africa haziwi mbaya namna hii ? Hata miaka ya nyuma ajali zilikuwa zinatokea lakini chuma haikuwa hivi. Pengine kuna lingine lakuzungumziwa hapa. Aina ya mabasi haya standard yake lazima ni ya chini sana na sasa abiria tunalipia. Hii ni sawa ? Poleni wafiwa. Wamiliki wa mabasi tuelezeni kwanini mnaruhusu gari bovu au dreva asiyeweza kupeleka bati kuendesha ? Hapa pana hitaji majibu kwa kweli.
    Sauti ya wanyonge

    ReplyDelete
  4. WATU WAACHE FIKRA FINYU ZENYE UNYANYAFUZI WA MAWAZO NA KILA BAADA YA AJALI WANASEMA AMRI YA MUNGU, NA AJALI HAINA KINGA!
    TUSIMLAUMU MWENYEZI MUNGU, TUFUNGUE MACHO NA KUTAFUTA NA KUPATA SULUHISHO MARA MOJA, NA AJALI INA KINGA,LESENI ZA KUNUNUA ZIISHE, MWENDO UPUNGUZWE, NA DEREVA AKIENDA MWENDO MKUBWA BASI ABIRIA WAMKALIE KOONI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...