Watu wawili Wanadaiwa kupoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa vibaya kufuatia ajali mbaya iliyotokea leo katika eneo la Sanangula nje kidogo ya mji wa Songea mkoani Ruvuma,ikilihusisha basi la Super Feo linalofanya safari zake kati ya Songea - Makambako lililoacha njia na kugonga mti. Aidha inaelezewa kuwa chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa ni mwendo kasi.
Sehemu ya basi hilo la Super Feo lionekanavyo pichani likiwa limepondeka pondeka baada ya kuacha njia na kugonga mti
Baadhi ya Wasomalia wema wakiwasaidia majeruhi waliopatwa na ajali ya basi hilo
Ee kweli Tanzania nimeamini kuna jinamizi la ajali. Mbona naiogopa Tanzania sasa kama sio nchi yangu? Ee Mungu tunakwenda wapi, jamani tumrudie Mungu nafikiri Mungu kachukia kwa uhuru tuliopewa na tunautumia vibaya. Mungu utusamehe dhambi zetu. Da!
ReplyDeleteMambo gani haya jamani mbona ajali zinatishia maisha.
ReplyDeleteHivi mbona mgari yana pondeka vibaya hivi? Hili linazua swala la usalaama wa vyombo vyetu. Ndiyo kusema mabasi haya ni kama mabati au ? Mimi nashangaa sana kuona mabasi yanayoishia kupondeka hivi. Mbona ajali kama hizi nchi nyingine tena Africa haziwi mbaya namna hii ? Hata miaka ya nyuma ajali zilikuwa zinatokea lakini chuma haikuwa hivi. Pengine kuna lingine lakuzungumziwa hapa. Aina ya mabasi haya standard yake lazima ni ya chini sana na sasa abiria tunalipia. Hii ni sawa ? Poleni wafiwa. Wamiliki wa mabasi tuelezeni kwanini mnaruhusu gari bovu au dreva asiyeweza kupeleka bati kuendesha ? Hapa pana hitaji majibu kwa kweli.
ReplyDeleteSauti ya wanyonge
WATU WAACHE FIKRA FINYU ZENYE UNYANYAFUZI WA MAWAZO NA KILA BAADA YA AJALI WANASEMA AMRI YA MUNGU, NA AJALI HAINA KINGA!
ReplyDeleteTUSIMLAUMU MWENYEZI MUNGU, TUFUNGUE MACHO NA KUTAFUTA NA KUPATA SULUHISHO MARA MOJA, NA AJALI INA KINGA,LESENI ZA KUNUNUA ZIISHE, MWENDO UPUNGUZWE, NA DEREVA AKIENDA MWENDO MKUBWA BASI ABIRIA WAMKALIE KOONI.