
MKurugenzi
wa Uzalishaji na Vipindi,Bwa.Ruge Mutahaba (Wanne kulia) kwa niaba ya uongozi wa
Clouds Media Group na PrimeTime Promotions Ltd ambao ndio waandaaji wa
Tamasha la Fiesta 2014,ametangaza rasmi kuwa onesho la tamasha hilo
lililobeba ujumbe murua kabisa wa sambaza upendo, litafanyika kesho
jumapili ndani ya uwanja wa Karume.
Tamasha hilo la Fiesta lilipangwa kufanyika JANA ijumaa mjini Musoma mkoani Mara lakini
kufuatia ajali mbaya iliyotokea mkoani humo jana na kusababisho vifo vya
watu zaidi ya 40,iliyotokea katika kijiji cha Sabasaba,wilaya ya
Butiama mkoani Mara lilisitishwa ili kwenda sambamba na tukio zima
katika kuwafariji wakazi wa Musoma na vitongoji vyake,kutoa mkono wa
pole,ambapo Wasanii waliotarajiwa kushiriki tamasha hilo na Waandaaji
walitoa msaada wa vifaa tiba kwa hatua za awali kusaidia majeruhi
waliokuwa wakipelekwa hospitali ya rufaa mjini Musoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...