Bw. Julius Mziray mkaguzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya Regency ya jijini Dar es salaam. Baada ya kumkamata mtu mmoja anayetuhumiwa kutumia kadi ya bima ya afya yenye namba 02-HCTP1801 ambayo inamilikiwa na Bw. Terry J. Maona kinyume na utaratibu.

Mtu huyo alikamatwa jana katika hospitali hiyo wakati akitaka kufanya vipimo vya (CityScan), ndipo mmoja wa wafanyakazi wa hospitali hiyo alipogundua na kupiga simu makao makuu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuwataarifu kuhusiana na tukio hilo, ambapo maofisa walifika na kukamata nyaraka hizo huku mgonjwa akitokomea kusikojulikana baada ya kugundulika, Bw. Julius Mziray amewaasa wamiliki wa kadi za Bima ya Afya kutozitumia watu tofauti badala yake zitumie kwa wahusika walioorodheshwa katika bima hiyo tu Jambo ambalo kuwaigiza katika mikono ya sheria na kupata adhabu kali. 2Bw. Julius Mziray mkaguzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF akiwasomea waandishi wa habari maelezo yaliomo katika nyaraka hizo 3 
Baadhi ya wgonjwa mbalimbali wakisubiri huduma katika hospitali hiyo 4 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa



  1. marekebisho= ni CT scan na sio city scan

    ReplyDelete
  2. Kutumia kadi ya bima isiyo yako ni kosa la jinai. Tukumbushane ili tuache kutaka huduma kutolewa bila malipo kwa sababu huduma zina gharama zake tukiendelea kutegemea bima ya afya kulipia gharama zisizokuwepo tunajiharibia wenyewe. Wakaguzi kuweni macho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...