Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiongea na wajumbe mbalimbali waliofika
katika uzinduzi wa kivuko cha kigamboni leo jijini Dar es Salaam kinachofanyiwa matenganezo na Jeshi la Wanamaji maeneo ya kurasini
,ambacho kinatarajiwa kuanza kutumika rasmi alhamisi wiki hii.
Mtendaji
Mkuu Temesa Injinia Marceline Magesa akitoa neno la shukrani kwa Jeshi la Wanamaji waliwezesha matengenezo
ya Mv Kigamboni leo jijini Dar es Salaam
ambapo kinatarajiwa kuanza kutumiwa na wananchi wiki hii.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli ( kushoto) na Katibu Mkuu
wa Ujenzi Injinia Mussa Iyombe(kulia)
wakisikiliza kwa makini maelekezo yaliyokuwa yakitolewa katika ufunguzi wa
kivuko cha Mv Kigamboni leo jijini Dar es Salaam kinachofanyiwa matenganezo na Jeshi la Wanamaji maeneo ya kurasini na kinatarajiwa kuanza kutumika wiki hii.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli ( katikati) akipata maelekezo
kutoka kwa Msimamizi wa matengenezo Luten Kanali Abel Gwanafyo (Kushoto), kulia ni Mkuu
wa Jeshi nla Maji Brigadia Jenerali Rostian Laswai wakati wa ufunguzi wa kivuko
hicho leo jijini Dar es Salaam ,amabapo
kinatarajiwa kuanza kutumika wiki hii kurahisisha usafiri kwa watu
wa Kigamboni.
Kivuko cha Mv Kigamboni kinavyoonekana kwa
ndani, kinatarajiwa kuanza kutumika siku ya alhamisi baada ya matengenezo
yalifanywa na Jeshi la Wanamaji kwa mda
wa wiki tatu tangu kilipoaacha kufanya kazi Agosti 14 mwaka huu.
Kivuko cha Mv Kigamboni kinavyoonekana upande wa mbele na ubavuni , kikiwa katika
hatua za mwisho tayari kwa kuanza
kutumiwa na wananchi siku ya alhamisi baada ya matengenezo yaliofanywa
na Jeshi la Wanamaji kwa mda wa wiki tatu
tangu kilipoaacha kufanya kazi Agosti 14 mwaka huu.( Picha na Lorietha Laurenc
eMaelezo).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...