Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni (pichani), anatarajiwa kuwasili nchini siku ya Jumatano asubuhi, tarehe 10 Septemba, 2014 kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Katika ziara hiyo nchini, Mhe. Museveni atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu, Dar es Salaam. Rais Museveni ataondoka baadaye siku hiyo hiyo kurejea nyumbani.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI,
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Karibu muheshimiwa rais.

    ReplyDelete
  2. Karibu nyumbani kwako mkongwe!!

    ReplyDelete
  3. Karibu sana Mzee Kaguta na ujisikie ya kana kwamba uko nyumbani. Ni kati ya wazee wachache sana tuliosaza katika miaka hii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...