Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia IMTU (IMTUSO), (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa kwa umma kufuatia maagizo ya Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) dhidi ya chuo cha IMTU. Kulia ni Naibu Naibu Waziri wa Mikopo na Ruzuku wa IMTU, Benson Lukwambe na Makamu wa Rais, Walter Nnko.

Na Dotto Mwaibale

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia IMTU wameiomba Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuunda tume maalumu itakayoshirikisha uongozi wa wanafunzi kufuatia utekelezaji wa maagizo waliyokiwekea chuo hicho ili kukamilisha kwa muda uliopangwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Rais wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho,IMTU (IMTUSO), Meekson Mambo alisema wanafunzi wa chuo hicho wana wasiwasi kuhusiana na muda wa miezi mitatu uliotolewa na  TCU kuhakikisha chuo cha IMTU kimekamilisha masharti yote waliyopewa vinginevyo kitafungwa.

"Matatizo ya chuo hicho ni ya muda mrefu hivyo kukiwa na kamati maalumu itasaidia kushughulikia suala hilo haraka na kulitafutia ufumbuzi badala ya kukifunga chuo hicho ambako kutaleta athari kubwa katika masomo kwa wanafunzi" alisema Mambo.


Mambo alisema TCU iunde kamati ya muda itakayoshirikiana na uongozi wa chuo uliopo sasa pamoja na uongozi wa wanafunzi waweze kusimamia na kuhakikisha kuwa maagizo ya TCU yanatekelezwa ili kutoa fursa kwa wanafunzi kuendelea na masomo huku mapungufu ya muda mrefu yaliyopo yakiendelea kutatuliwa kwani muda huo wa miezi mitatu waliopewa ni mdogo.

Aliongeza kuwa endapo uongozi wa chuo utashindwa kutekeleza maagizo ya TCU hawaungi mkono hoja ya kufunga chuo badala yake kiwekwe chini ya serikali au chuo kikuu kingine ambacho kina kitakuwa na uwezo wa kusimamia mfano Chuo Kikuu cha Dar es Salaa ambacho hakina kitivo cha afya.

Makamu wa Rais wa Serikali ya chuo hicho, WalterNnko alisema kukifunga chuo hicho kutawaathiri wanafunzi zaidi ya 1000 waliopo chuoni hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ni muhimu kuangalia mustakabali wa wanafunzi walioko katika chuo hicho wakati maamuzi yanapotolewa. Hata kama uamuzi ungekuwa kukifunga basi kuwe na utaratibu uliowekwa kwa ajili ya kupelekwa wanafunzi waliopo ambao hawajamaliza masomo yao.

    ReplyDelete
  2. Naunga mkono hoja ya Anonymous hapo juu.Nadhani kuna adhabu nyingi Serikali inaweza kuzichukua (kuwatoza fani etc) bila kuathiri elimu ya wanafunzi, ajira za wafanyakazi etc, ambao hawahusiki moja kwa moja na makosa ya uongozi wa chuo.

    ReplyDelete
  3. hao wanafunzi nani aliwambia wakasomee vyuo vya kata.

    Muhimbili hawakuiona? au hawakuwa na divisheni nzuri?

    kila ukifanya kosa utakutana nalo mbele.

    ReplyDelete
  4. Fikiria kabla ya kutoa hoja yako.hao wanafunzi wameomba tcu na tcu ndio iliyowapeleka hapo.usikurupuke tu kutoa maoni yasiyo na msaada wowote,kama huna mchango wa maana sio lazima kuchangia mada.

    ReplyDelete
  5. TCU iwe inaangalia kabla ya kutoa maamuzi yake kwan kulikimbia tatizo siyo kulitatua ila nikulipumzisha. Unapo kinyima chuo udahili wa wanafunzi tena hususani kwa mwaka wa masomo 2014/2015 ambapo kiasi cha ufaulu kimeongezeka je? wanafunzi wakasome wapi wale ambao kozi zao zinapatikana katika chuo cha IMTU. Mimi naimbo serikali itoe tamko la kukiruhusu chuo cha IMTU KUENDELEA NA UDAHILI WA WANAFUNZI kama kawaida wakati mambo mengine yanaendelea

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...