SAM_0646Engineer Carlos Mkindi ambaye ni mkurugenzi wa mkundi production akiongea na vyombo vya habari kuhusiana na Tamasha kubwa la upendo kwa mama linalotarajiwa kufanyika jijini Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid tarehe 02-11-2014
SAM_0669
Engineer Carlos Mkindi ambaye ni mkurugenzi wa mkundi production akiongea na wanahabari kuhusiana na Tamasha la Upendo kwa mama ambalo linalenga kutoa mitaji kwa zaidi ya akina mama 50 wajasiriamali ili kuwawezesha kujiajiri pamoja na kuwaombea na kuwashukuru kwa moyo wa upendo waliyonayo kwa kujitoa katika kusimamia familia na malezi
SAM_0670
Mratibu wa Tamasha la Upendo kwa mama Bw. Linus Kilembu akiongelea maandalizi ya Tamasha kuwa limekamilika kwa asilimia 90
SAM_0675
Engineer Carlos Mkindi mwenyekiti wa Tamasha la upendo  ambaye ni mkurugenzi wa mkundi production akifanyiwa mahojiano na wanahabari katika studio za mkundi production zilizopo njiro mkoani Arusha
SAM_0676
Kampuni ya Makundi Production ya jijini Arusha iko katika maandalizi ya kufanya tamasha kubwa la aina yake litakalo julikana kwa jina la UPENDO WA MAMA ambalo linatarajiwa kufanyika tarehe 02 Novemba 2014 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid.
 
Tamasha hilo litaongozwa na waimbaji wa Nyimbo za Injili wakubwa kutoka Kenya, Sara K, na Cristina Shusho kutoka Tanzania, huku likipambwa na Ambwene Mwasongwe, Baraka Maasa, Eng calros Mkundi, Ester Bukuku, Matha Mwaipaja, Nesta sanga, Meth Chengula, Matumaini, Eline Patrick bila kuwasahau waimbaji wengine kutoka Mkoani Arusha pamoja na Kwaya Mbalimbali.
 
Lengo la tamasha hilo la UPENDO KWA MAMA linalengo la kutoa Mitaji kwa zaidi ya akina mama 50 wajasiriamali ili kuwaongezea uwezo wa kujiajiri, vilevile utakuwa ni wakati mwafaka wa kuwashukuru wakinamama wote kwa upendo waliyonao ukiambatana na kujitolea katika kusimamia Familia na malezi ya watoto.
 
Studio ya Mkundi nakamati ya maandalizi ya Tamasha la UPENDO KWA MAMA wanatoa nafasi kwa watanzania, Taasisi na Mashirika yote ambayo yako tayari kuungana na Studio ya Mkundi kwa Ufadhili wa hali na mali ili kufanikisha tamasha hili la UPENDO KWA MAMA.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog Arusha)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...