Na: Geofrey Tengeneza
Shirika la hifadhi la taifa (TANAPA) kwa kushirikiana na mamlaka ya hifadhi ya
eneo la Ngorongoro pamoja na shirika la ndege la Ethiopia wamedhamini onesho
la kimataifa ya utalii lijulikanalo kama ‘Swahili International Tourism Expo’ (S!
TE).
Taasisi hizo tatu zinakuwa ndio wadhamini wakuu wa maonesho hayo ya kimataifa
ya utalii ya kwanza Tanzania yanayoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania kwa
kushirikiana na kampuni ya Pure Grit Project and Exhibition Management
Ltd ya Afrika Kusini ambao pia ndio waandaji wa onesho la utalii la INDABA
linalofanyika kila mwaka Afrika Kusini.. Onesho hili la kwanza la S!TE
litafanyika kuanzia mwezi Oktoba, tarehe 1 – 4, 2014 katika ukumbi wa mikutano
Mlimani City. Pamoja na maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali za utalii
lakini pia kutakuwa na maonesho ya utalii wa utamaduni wa mtanzania.

Aidha
sambamba na maonesho kutakuwa pia na kongamano kwa muda wa siku zote nne
ambapo mada mbalimbali kuhusu utalii zitawasilishwa na wataalamu katika sekta
ya utalii na kujadiliwa.
Onesho hili la utalii la kimataifa ambalo lmelenga watalii wanaokuja Afrika
yanatarajia kuvuta maelfu ya wasafirishaji wakubwa wa watalii na wadau wa
sekta ya kitalii na usafiri kutoka kila pande za Dunia. Kama sehemu ya udhamini
wake, licha ya mashirika mengine, shirika la ndege la Ethiopia ndilo litakuwa
wasafirishaji wakubwa wa watalii na wandishi wa habari wa kimataifa kutoka nchi
mbalimbali duniani zikiwemo Marekani, Uingerza, Ujerumani n.k wanaokuja kwa
ajili ya onesho hili.
S!TE litakalo kuwa likifanyika kila mwaka mwezi Oktoba, litachukua muundo wa
maonesho ya kiusafiri na kibiashara likilenga pia katika kuonyesha utalii endelevu
wa kisasa, uhifadhi na mambo mengine yanayohusiana na masoko ya utalii.

Ni ukweli usiopingika kwamba Tanzania imebeba vivutio mbalimbali vya kitalii
kama vile mlima Kilimanjaro, Zanzibar na hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Kwa
ujumla Tanzania inaweza tu kuitwa kitovu cha vivutio vya asili Afrika kwani
Tanzania ndio nchi pekee yenye vivutio vitatu kati ya saba vya asili barani afrika
ambavyo ni Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu kuliko yote barani afrika;
Ngorongoro Crater ambayo ni kubwa duniani isiyomomonyoka, na hifadi ya
Taifa ya Serengeti, maarufu kwa nyumbu wanaohama wakiwa katika makundi
makubwa na misururu mirefu kutoka kusini kuelekea kaskazini na kurejea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...