Makamu wa Rais wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Madini ya Vito – Thailand, ambao ndiyo waandaaji wa Maonesho ya Vito ya Bangkok, Tony Brooks akizungumza na baadhi ya Watanzania wanaoshiriki katika Maonesho hayo nchini Thailand alipotembelea Banda la Tanzania.
Mkuu wa Banda la Tanzania katika Maonesho ya Vito ya Bangkok ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT), Archard Kalugendo akimweleza mdau wa madini ya vito aliyetembelea banda hilo kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania. Mbele yao ni vinyago vilivyochongwa kutokana na miamba.
Mfanyabiashara wa madini ya vito kutoka Tanzania, Peter Pereira akimhudumia Mteja aliyefika katika Banda la Tanzania kwenye Maonesho ya Vito ya Bangkok. Maonesho hayo ya siku tano yalianza Septemba 9 mwaka huu.
Mfanyabiashara wa madini ya vito kutoka Tanzania, Latifah Abdallah akitoa maelezo kuhusu madini hayo kwa wadau waliotembelea Banda la Tanzania katika Maonesho ya Vito ya Bangkok.
Mchimbaji mdogo wa madini ya vito, Kassim Idi Pazi akihudumia wateja waliotembelea Banda la Tanzania katika Maonesho ya Vito ya Bangkok.
Baadhi ya Washiriki kutoka Tanzania katika Maonesho ya Vito ya Bangkok wakipozi kwa picha muda mfupi kabla ya kuanza kwa siku ya tatu ya maonesho hayo. Kutoka Kushoto ni Asimwe Kafrika, Iddi Pazzi, Gregory Kibusi, Nelson Magawa, Teddy Goliama na Matiko Sanawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...