Meneja
Mahusiano wa Mgodi wa North Mara Bi
Fatuma Mssumi (mbele) akielezea shughuli za mgodi wa North Mara mbele ya jopo
la majaji waliotembelea mgodi huo ili kuendelea na zoezi lake la kumtafuta
mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji.
Afisa
Mahusiano wa Mgodi wa North Mara Bw. Zakayo Kalebo (wa tatu kutoka kushoto)
akielezea mchango wa mgodi wa North Mara katika ujenzi wa nyumba za wauguzi wa zahanati ya Matongo (zinazoonekana
nyuma) mbele ya timu ya majaji na sekretarieti iliyotembelea mradi wa nyumba
hizo. Mradi wa nyumba hizo uligharimu
Dola za Marekani 100,000.
Afisa
Uhusiano wa Kijiji cha Matongo Bw. Magesa
Wanjara akionesha jinsi ya kutumia bomba la kisima cha maji
kilichofadhiliwa na mgodi wa North Mara
mbele ya timu ya majaji, sekretarieti na
wajumbe wengine.
Afisa
Mahusiano wa Mgodi wa North Mara Bw. Zakayo Kalebo ( wa tano kutoka kushoto)
akielezea mchango wa mgodi wa North Mara katika uwezeshaji wa kikundi cha
vijana katika mradi wa kitalu cha mboga za majani, mbele ya majaji na
sekretarieti iliyotembelea kitalu hicho. (kinachoonekana kwa nyuma).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...