Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Chifu Kishosha Mabiti (wa tatu kutoka kulia)
akimwonesha Mwenyekiti wa Jopo la Majaji kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo
ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji Prof. Samwel Wangwe (wa pili kutoka
kushoto) ramani ya kijiolojia ya mkoa huo mara timu hiyo ilipomtembelea ofisini
kwake.
Mkuu wa wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza Mhe. Mariam Lugaila (mbele kwa
mbali) akizungumza na jopo la majaji na sekretarieti kwa ajili ya kumtafuta mshindi
wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji iliyomtembelea ofisini kwake
kabla ya kuanza zoezi hilo katika wilaya yake.
Afisa Madini Mkazi wa Bariadi Bw. Nyaisara Mgaya ( wa pili kutoka kushoto)
akimwonesha Mwenyekiti wa Jopo la Majaji kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo
ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji Prof. Samwel Wangwe (kulia) moja
ya aina ya mawe yenye madini ya ulanga kwenye ofisi za kampuni ya utafutaji wa
madini hayo ya African Eagle Resource Ltd.
Mtaalamu kutoka katika kampuni ya Kassco Limited inayojihusisha na madini ya
ujenzi Bw. Japhes Gerase (kulia) akielezea mchango wa kampuni yake katika
ukarabati wa shule ya msingi ya Ntende (inayoonekana pichani) majaji, sekretarieti
na wajumbe waliofanya ziara katika shule hiyo.
Mtaalamu kutoka katika kampuni ya Kassco Limited inayojihusisha na madini ya
ujenzi Bw. Japhes Gerase (kulia) akionesha moja ya kisima kilichochimbwa na
kampuni hiyo kwa ajili ya wakazi wa kijiji cha Ntende mbele ya timu ya majaji na
sekretarieti iliyotembelea visima hivyo kama moja ya ufanyaji ya tathmini ya miradi
iliyofadhiliwa na kampuni hiyo.
Mmoja wa wajumbe wa timu ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za
Jamii na Uwezeshaji Mhandisi Moses Ndalahwa (kushoto) akiwahoji vijana wa kijiji
cha Ntende kuhusiana na mchango wa makampuni ya madini ya ujenzi katika kijiji
hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...