Chama cha Ujenzi wa Taifa cha NRA ,(National Reconstruction Alliance); kinatoa salamu za pole/rambirambi kwa Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mhe Jakaya Kikwete, Waziri za Uchukuzi, Mkuu wa mkoa wa Mara na Wafiwa kwa ajali mbaya ya Basi iliyopelekea kupotea kwa maisha ya watanzania zaidi ya 40, akiongea kwa njia ya simu akiwa katika ziara ya kikazi mkoani  kigoma Naibu KATIBU MKUU NA KATIBU MKUU wa BODI ya chama Mhe Hassan Kisabya (pichani) , ametoa salamu hizo kwa niaba ya Chama chake.

Mhe kisabya amesema, amepokea kwa masikitiko na mstuko Mkubwa taarifa za ajali hiyo,na kuongeza kuwa ,ajali ni miongoni kwa majanga makubwa kitaifa yanayopoteza maisha ya watanzania na kuwaomba madereva kuwa waangalifu wakati wate ili kuokoa nguvu kazi ya taifa.
Pia ,amewataka walinzi wa usalama barabarani kuongeza juhudi ili kuzuia ajali hizo.
Mhe Hassan Kisabya, Amewataka wafiwa kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu na kuacha wahusika kufanya kazi Yao ya uchunguzi wa ajaili hiyo KISHERIA.
Mhe kisabya,pia amezitaka kampuni husika za mabasi kuhakikisha wanaajiri madereva wenye sifa ili kuifanya huduma hii ya usafiri wa mabasi kuwa kimbilio la wengi kwa kuwa njia hii Ndio imekuwa nafuu na haraka na inawafaa watu wa hali zote.
Katika salamu hizo, mhe kisabya ameomba watanzania hususani wasafiri kutoa taarifa kwa vyombo husika pale wanapokuwa na mashaka na uendeshaji wa dereva wawapo safarini ili kuwa msaada kwa  wasimamizi wa usalama wao,hasa tukizingatia ulinzi na usalama ni jukumu letu sote(ibara ya 26(1),(2) ya katiba ya Tanzania ,1977),pia UTII WA SHERIA BILA SHURUTI unatutaka kuwajibika  na kuifanya Tanzania kuwa mahala salama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...