Mkurugenzi wa Afya katika Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Dkt. Sarah Maongezi akiongea wakaati wa ufunguzi wa mkutano wa uragibishi wa saratani ya shingo ya kizazi na matiti kwa akina mama unaofanyika Hoteli ya Courtyard hapa Da es Salaam tarehe 11.9.2014.
Dkt. Williama Kafura akifungua rasmi mkutano wa uragibishi wa saratani ya mlango wa kizazi na matiti kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kwa akina mama katika nchi za Afrika Mashariki.
Katibu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Ndugu Daud Nassib akitoa salamu za Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwa wajumbe wa mkutano wa siku tatu wa saratani ya shingo ya kizazi na matiti kwa akina mama.
Washiriki wa mkutano wa saratani kwa akina mama wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi Dkt. William Kafura aliyemwakilisha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii aliyefungua rasmi mkutano huo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa uragibishi (advocacy) kuhusu saratani ya shingo ya kizazi na matiti kwa akina mama kutoka katika nchi za Afrika Mashariki. Mkutano huo pia unahudhuriwa na wajumbe kutoka Zambia, Malawi, Madagascar na Zimbabwe. Katika picha wanaonekana wajumbe wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa. Mkutano huo wa siku tatu unafanyika katika hoteli ya Courtyard hapa Dar Es Salaam na umeandaliwa kwa pamoja kati ya WAMA na Shirika la WE CAN (Women Empowerment Cancer Advocacy Network) kutoka nchini Marekani. PICHA NA JOHN LUKUWI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...