Baadhi ya wadau wa afya wakifuatilia uzinduzi wa wa Mpango wa Maboresho kwa Wafanyakazi
wa Sekta ya Afya (HRHSP 2014/2019), uliofanyika Dar es Salaam jana. Picha na Joseph Zablon.
Wafanyakazi katika sekta ya afya wanadaiwa
kutumia muda wa asilimia 20 na isiyozidi 30 kwa mwa mwezi
jambo ambalo ni kinyume chja mikataba yao ya ajira inayowataka
kuwepo kazini hadi saa nane hivyo kukwamisha Mpango wa
Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid alisema hayo
wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Maboresho ya Wafanyakazi wa
Sekta ya Afya 2014/2019 ambao upo chini ya wahisani wa Global
Fund, kupitia shirika la Misaada la Japani (Jica).
Alibainisha kuwa wafanyakazi katika sekta ya afya wanatumia
asilimia 20 na isiyozidi 30 kwa mwezi katika kufanyakazi ambazo
hazihusiani na ajira zao jambo ambalo linasikitisha na kukwaza
jitihada za serikali katika sekta hiyo.
Dk Rashid alisema chini ya utaratibu wa BRN, serikali imefanikiwa
kuvuka lengo la kusomesha na kuwandaa watalaam katika kada
tofauti za afya na awali ilikuwa wawe wamefikia 10,000 hadi kufika
2017 kutoka idadi ya mwaka 2013 ya wahitimu 3,000 lakini lengo
hilo hadi sasa limeishavukwa.
“Hadi hivi sasa tumeishahitimisha wanafunzi 10,700 hivyo kupitia
mpango huu ambao tumeuzindua leo tayari tumevuka malengo
hivyo tutapanga mapya kuelekea 2017” alisema na kuongeza kuwa
mpango wa BRN hautaangalia wingi wa idadi na mgawanyiko
pekee wa raslimali watu.
Alisema hivi sasa mpango uliopo ni kuhakikisha wale ambao
wamepangiwa vituo vya kazi wanafika na ku muda ambao
wanatakiwa wawepo na sio tofauti na hivyo.
Awali akizungumza wakati wa uzinduzi wa program hiyo,
Mkurugenzi wa Mafunzo na Maendeleo ya Raslimaliwatu katika
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Otilia Flavian Gowelle
alisema pia kuna ambao wanakacha kwenda vituo vya kazi
walivyopangiwa.
Alisema asilimia 60 ya waliopangiwa sehemu za kufanyiakazi
hawaendi katika kwa visingizo mbalimbali na kubadilisha dakika za
mwisho na mipango inafanywa ili wahitimu hao wa ngazi ya kati
katika sekta ya afya wawe na mikataba na serikali ya kufanyakazi
miaka mitatu kabla ya kwenda kwingineko.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...