Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akiwa ndani ya moja ya nyumba
za Wakimbizi waliopo katika Kituo cha Mpito cha Wakimbizi (NMC) kilichopo mjini Kigoma.
Katika nyumba hiyo Waziri Chikawe alizungumza na familia ya mkimbizi kutoka nchini Kongo
(kushoto) wanaoishi katika nyumba hiyo. Waziri Chikawe yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
Wapili kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi
(UNHCR), Joyce Mends-Cole. Kituo hicho kilichopo mjini humo kinawahifadhi wakimbizi zaidi ya
400 wakiwemo wanaoenda kwenye matibabu, wanaoenda nchi ya tatu, wenye matatizo ya kiusalama,
na waomba hifadhi ya muda ya ukimbizi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akiangalia jiko ambalo linatumika
kupikia chakula cha wakimbizi katika Kituo cha Mpito cha Wakimbizi (NMC) kilichopo mjini
Kigoma. Katikati ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi
(UNHCR), Joyce Mends-Cole. Waziri Chikawe yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi. Kituo
hicho kilichopo mjini humo kinawahifadhi wakimbizi zaidi ya 400 wakiwemo wanaoenda kwenye
matibabu, wanaoenda nchi ya tatu, wenye matatizo ya kiusalama, na waomba hifadhi ya muda ya
ukimbizi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimsalimia mkimbizi kutoka nchini
Kongo aliopo katika Kituo cha Mpito cha Wakimbizi (NMC) kilichopo mjini Kigoma. Waziri
Chikawe na maafisa wake wapo mkoani Kigoma kwa ajili ya ziara ya kikazi. Kituo hicho kilichopo
mjini humo kinawahifadhi wakimbizi zaidi ya 400 wakiwemo wanaoenda kwenye matibabu,
wanaoenda nchi ya tatu, wenye matatizo ya kiusalama, na waomba hifadhi ya muda ya ukimbizi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akiwasalimia waimba kwaya
wakimbizi kutoka nchini Kongo waliopo katika Kituo cha Mpito cha Wakimbizi (NMC) kilichopo
mjini Kigoma. Waimba kwaya hao walimpokea Waziri Chikawe kwa nyimbo mbalimbali wakati
alipotembelea Kituo hicho cha mpito. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole. Waziri Chikawe yupo mkoani Kigoma kwa
ziara ya kikazi. Kituo hicho kilichopo mjini humo kinawahifadhi wakimbizi zaidi ya 400 wakiwemo
wanaoenda kwenye matibabu, wanaoenda nchi ya tatu, wenye matatizo ya kiusalama, na waomba
hifadhi ya muda ya ukimbizi. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...