Kampuni ya simu za Mkononi ya Bharti
Airtel yenye kufanya shughuli zake katika nchi 20 barani Afrika na
Asia leo imetangaza mpango wa kuzindua huduma ya kutuma na kupokea
pesa Afrika Mashariki.
Huduma hii ya kwanza barani Afrika itamwezesha
Mteja wa Airtel kutuma , kupokea na kutoa pesa kutoka kwenye salio
lake la Airtel Money
Hatua ya awali ya huduma hii inategemea kuanza tarehe 1 November 2014
kwa kushirikisha nchi za Kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda ambapo
huduma hii itaweza kupatikana kufatia kibali kutoka benki kuu ya
serikali ya Rwanda, Kenya, Tanzania na Uganda cha kuendelea na
uzinduzi wa mpango huu.
Hatua ya pili ya mwendelezo wa mpango huu kwa
nchi nyingine za Afrika ambapo Airtel inaendesha biashara yake
zinategemea kuanza mwakani.
Akiongea wakati wa Mkutano wa Biashara kwa wakuu wa Makampuni katika
nchi za Afrika Mashariki uliyofanyika Rwanda, Mkurugenzi na Mkuu wa
kitengo cha Airtel Money bw, Chidi Okpala,alisema” hii ni hatua muhimu
itakayowawezesha wateja wetu kuondoa vikwazo vya kutuma na kupokesa
pesa nje ya mipaka ya nchi zao kiurahisi kuweza kufanya hivyo kwa
kupitia huduma ya Airtel Money.
Huduma hii itatanua wigo, kutoa unafuu
na kuleta urahisi kwa wafanyabiashara wadogo kufanya malipo ndani na
nje ya mipaka ya nchi za Afrika Mashariki.”
Aliongeza kwa kusema “huduma hii pia italeta fulsa za kibiashara, ni
wazi kwamba huduma za kifedha kupitia simu ni muhimili mkuu katika
ushirikiano wa huduma za kifedha na ndio dhamira ya serikali za
Rwanda, Uganda, Kenya na Tanzania katika kuhakikisha inakuza shughuli
za kibiashara ndani ya nchi za Afrika Mashariki.”
Sambamba na hilo Hatua hii ya kwanza ya uzinduzi wa huduma hii pia
itawawezesha wateja wa Benki ya Afrika nchini Kenya na Uganda kutuma
na kupokea pesa katika nchi hizi mbili.
Huduma ya Airtel money ni huduma ya kifedha kupitia simu ya mkononi
iliyo salama na rahisi inayowawezesha wateja kutuma pesa kutoka simu
moja kwenda kwenye simu za mitandao yote, pia inamuwezesha mteja
kununua muda wa maongezi kwaajili ya simu yake au kwa simu ya mtu
mwingine.
Pia inawawezesha wateja kulipa ankra zao mbalimbali na
kutoa pesa katika mashine za (ATM)’s
Imekaririwa na jumuiya ya Afrika Masharika kwamba huduma za kifedha
kupitia simu za mkononi ni muhimu katika nchi hizi kutokana na
urahisi, uharaka na inaokoa muda kwa wateja na wafanyabiashara.
Uzinduzi wa huduma za kibunifu kama vile za mikopo, kuweka pesa, na
kutoa huduma za bima zinazofanywa kwa kushirikiana na makampuni
yanayotoa huduma za kibenki zimeleta mabadiliko chanya na kuongeza
kasi ya ushirikiano wa kuvuka mipaka ya nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...