Balozi Sefue akishangiliwa na kina mama wa DICOTA waliokuwa wamevalia sare kumkaribisha kufungua Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Baraza la Watanzania waishio Marekani (DICOTA 2014) Mkutano huo wa siku tatu unafanyika katika Hoteli ya Millenium mjini Durham, North Carolina. 
Balozi Sefue akizungumza na Meya wa Durham, Mhe. Bell
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akifungua rasmi Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Baraza la Watanzania waishio Marekani (DICOTA 2014) Mkutano huo wa siku tatu unafanyika katika Hoteli ya Millenium mjini Durham, North Carolina. Washiriki kwenye mkutano huo ni pamoja na Watanzania kutoka Majimbo mbalimbali ya Marekani, Wajumbe kutoka Serikalini na Sekta Binafsi na Serikali ya Marekani. Katika hotuba yake ya ufunguzi Balozi Sefue alilipongeza Baraza la DICOTA kwa juhudi na mafanikio mbalimbali na pia alisema Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi hizo.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula (mwenye scarf) kwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo, Mwalimu Christopher Mwakasege na Wajumbe wengine wakimsikiliza Balozi Sefue (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa DICOTA 2014
Balozi Mulamula akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa DICOTA 2014
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...