Jeshi la polisi katika Kanda maalum ya Dar es Salaam limetumia maji ya kuwasha kuwatawanya wafuasi wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) waliokuwa wakijiandaa KUANDAMANA hadi Ikulu.


Aidha, jeshi hilo limemkamata Mwenyekiti wa BAWACHA, Mhe. Halima Mdee aliyekuwa akiyaongoza maandamano hayo.

BAWACHA walipanga kuandamana hadi Ikulu ya Dar es Salaam kwa nia ya kuonana na Rais Jakaya Kikwete ili kumsishi asisaini Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, ambayo ilipitishwa na Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba siku ya Alhamisi mkoani Dodoma.

Jeshi la Polisi lilizuia maandamano hayo kupitia taarifa yake iliyoitoa hapo jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...