Meneja
Biashara wa Bayport Tanzania, Thabit Mndeme kushoto; na Meneja Masoko
na Mawasiliano (katikati), Ngula Cheyo waki zinduwa Mkopo wa Bidhaa,
Bayport Head office Daressalaam.
===== ===== =====
TAASISI ya kifedha ya Bayport Tanzania, leo imezindua huduma
mpya ijulikanayo kama Mikopo ya Bidhaa ikiwa na lengo la kurahisha utendaji
kazi wa watumishi wa umma na wafanyakazi wote wa kampuni zilizoidhinishwa na
Bayport.
Uzinduzi huo uliofanyika jana, umeonyesha matumaini mapya ya
Watanzania wanaosumbukia usafiri katika vituo vyao vya kazi, hususan maeneo ya
mikoani ambako mara kadhaa kumesikika malalamiko ya maisha magumu ya watumishi
wa umma.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja Biashara wa
Bayport Tanzania, Thabit Mndeme, alisema kwamba
ni wakati wa kukuza uchumi wan chi kwa kuhakikisha kuwa watu wote
wanafanya kazi kwa bidii na shauku yote.
Alisema wapo watumishi ambao wanaishi kwa tabu kutokana na
changamoto ya usafiri na mahitaji mengine ya kijamii, hivyo kwa kupatikana
hudumaa mpya ya kukopeshwa pikipiki bodaboda ni jambo zuri kwao.
‘’Bayport tumekaa na kuangalia namna gani Watanzania
wataendelea kufanya kazi kwa moyo na kukuza uchumi wetu, tukaona sambamba na
kuwakopesha fedha kama tunavyofanya, pia tuwakopeshe bidhaa kama vile Boxer,
Toyo na Lifan.
‘’Zote hizi zitakuwa kwenye mpangilio mzuri sambamba na
kuzikatia huduma ya bima, kuzifanyia servise mara tatu bure, garantii ya mwaka
mmoja, huku mkopaji akitakiwa kulipa kwa miezi 36 sawa na miaka mitatu,’’alisema
Mndeme.
Naye Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Tanzania, Ngula
Cheyo, alisema kuwa mikopo hiyo mipya itapatikana kwa masaa 24, huku ikipatikana
pia kwa mikoa yote na wilaya zote kwenye ofisi za Bayport Tanzania.
‘’Tunawaomba watu waendelee kuiunga mkono Bayport kwa
kuhakikisha kuwa wanachangamkia fursa hii ya mikopo ya bidhaa ambayo
tumeianzisha ili kuwafanya watumishi wa umma na wafanyakazi wengine
warahisishiwe utendaji wao wa kazi,’’ alisema Cheyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...