Na Mwandishi Maalum, New York
Inaweza ikawa ni taarifa za kushangaza kuwa hata mkaa ambao ni nishati
inayotumiwa na jamii kubwa sehemu mbalimbali hususani Barani Afrika kwamba
mapato yatokanayo na biashara hiyo yanaweza kuwa chanzo ya mapato kwa
makundi ya kigaidi.
Taarifa kwamba mapato yatokanayo na mkaa yanatumika ndivyo sivyo, zimejidhihirisha
mwishoni mwa wiki ( Ijumaa ) pale Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa
lilipopitisha kwa kura Azimio namba 2182 la mwaka 2014 ambalo pamoja na mambo
mengine linaweka vikwazo na kupiga marufuku biashara haramu ya mkaa huko
Somalia.
Upigaji marufuku hiyo na vikwazo dhidi ya biashara ya mkaa inatokana na kile
kilichoelezwa wakati wa mkutano wa Baraza , kwamba kundi la kigaidi la Al-
Shabaab limekuwa linanufaika na biashara hiyo kwa kuchukua sehemu ya mapato .
Azimio hilo lilipita kwa kura 13 za kuliunga mkono huku wajumbe wawili Jordan na
Urusi wakipiga kura ya kutoegemea upande wowote. Baraza linawajumbe 15 ambapo
watano kati yao wanakura ya veto.
Vikwazo dhidi ya Biashara haramu ya mkaa kutoka Somalia iliwekwa kwa mara ya
kwanza mwaka 2012 kwa azimio 2036. Na kwamba tangu kuwekwa kwa vikwazo
hivyo kumekuwapo na ongezeko la biashara hiyo ya mkaa kiasi cha kuifanya Serikali
ya Mpito nchin humo kulalamika kwa Baraza la Kuu la Usalama.
Baadhi ya wajumbe waliozungumza baada ya kupitishwa kwa Azimio hilo ambalo pia
linaongeza muda wa vikwazo vya silaha, wameeleza kuwa kundi la Al-Shabaab
linapata theruthi moja ya mapato yanayotokana na biashara hiyo ambayo inaeelezwa
kuwa thamani yake ni dola za kimarekani 250 milioni.
Kupitia Azimio hilo Baraza linatoa wito kwa wadau mbalimbali zikiwamo nchi
zinazochangia walinzi wa Amani nchini Somalia, kupitia AMISOM kutoa ushirikiano
katika kudhibiti biashara hiyo .
Aidha Azimio linatilia mkazo wa ukaguzi wa meli zinazopita katika mwambao wa pwani
ya Somalia na zile zinazopita katika kina kirefu. Na hasa pale inapohisiwa kwamba
huenda zikawa zimebeba bidhaa hiyo au silaha na zana nyingine za kivita ambazo
zinadhibitiwa kupita Azimio hilo. Na kwamba bidhaa hizo zikikamatwa basi viharibiwe
mara moja.
Pamoja na Azimio kutilia mkazo vikwazo dhidi ya biashara hiyo ya mkaa, biashara
ya haramu ya silaha na au uingizaji wake. Pia limeongeza muda wa mamlaka kwa
Walinzi wa Amani wanaohudumu chini ya Umoja wa Afrika ( AMISOM) hadi mwaka
2015.
Walichotakiwa ni kupiga marufuku mkaa uliozalishwa na magaidi na sio kuzuia kazi halali inayoweza kufanya na raia wema.
ReplyDeleteYaani magaidi wamewashinda mpaka wanaweka vikwazo ambavyo ni kuwagaidi raia wema.
sheria ambayo ikitekelezwa itamdhuru raia mwema ni si ya kimaadili mema.