Na Mwandishi Maalum, New York

Inaweza ikawa ni taarifa za kushangaza kuwa hata mkaa ambao ni nishati inayotumiwa na jamii kubwa sehemu mbalimbali hususani Barani Afrika kwamba mapato yatokanayo na biashara hiyo yanaweza kuwa chanzo ya mapato kwa makundi ya kigaidi.

Taarifa kwamba mapato yatokanayo na mkaa yanatumika ndivyo sivyo, zimejidhihirisha mwishoni mwa wiki ( Ijumaa ) pale Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipopitisha kwa kura Azimio namba 2182 la mwaka 2014 ambalo pamoja na mambo mengine linaweka vikwazo na kupiga marufuku biashara haramu ya mkaa huko Somalia.

Upigaji marufuku hiyo na vikwazo dhidi ya biashara ya mkaa inatokana na kile kilichoelezwa wakati wa mkutano wa Baraza , kwamba kundi la kigaidi la Al- Shabaab limekuwa linanufaika na biashara hiyo kwa kuchukua sehemu ya mapato . Azimio hilo lilipita kwa kura 13 za kuliunga mkono huku wajumbe wawili Jordan na Urusi wakipiga kura ya kutoegemea upande wowote. Baraza linawajumbe 15 ambapo watano kati yao wanakura ya veto.

Vikwazo dhidi ya Biashara haramu ya mkaa kutoka Somalia iliwekwa kwa mara ya kwanza mwaka 2012 kwa azimio 2036. Na kwamba tangu kuwekwa kwa vikwazo hivyo kumekuwapo na ongezeko la biashara hiyo ya mkaa kiasi cha kuifanya Serikali ya Mpito nchin humo kulalamika kwa Baraza la Kuu la Usalama.

Baadhi ya wajumbe waliozungumza baada ya kupitishwa kwa Azimio hilo ambalo pia linaongeza muda wa vikwazo vya silaha, wameeleza kuwa kundi la Al-Shabaab linapata theruthi moja ya mapato yanayotokana na biashara hiyo ambayo inaeelezwa kuwa thamani yake ni dola za kimarekani 250 milioni.

Kupitia Azimio hilo Baraza linatoa wito kwa wadau mbalimbali zikiwamo nchi zinazochangia walinzi wa Amani nchini Somalia, kupitia AMISOM kutoa ushirikiano katika kudhibiti biashara hiyo .

Aidha Azimio linatilia mkazo wa ukaguzi wa meli zinazopita katika mwambao wa pwani ya Somalia na zile zinazopita katika kina kirefu. Na hasa pale inapohisiwa kwamba huenda zikawa zimebeba bidhaa hiyo au silaha na zana nyingine za kivita ambazo zinadhibitiwa kupita Azimio hilo. Na kwamba bidhaa hizo zikikamatwa basi viharibiwe mara moja.

Pamoja na Azimio kutilia mkazo vikwazo dhidi ya biashara hiyo ya mkaa, biashara ya haramu ya silaha na au uingizaji wake. Pia limeongeza muda wa mamlaka kwa Walinzi wa Amani wanaohudumu chini ya Umoja wa Afrika ( AMISOM) hadi mwaka 2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Walichotakiwa ni kupiga marufuku mkaa uliozalishwa na magaidi na sio kuzuia kazi halali inayoweza kufanya na raia wema.

    Yaani magaidi wamewashinda mpaka wanaweka vikwazo ambavyo ni kuwagaidi raia wema.

    sheria ambayo ikitekelezwa itamdhuru raia mwema ni si ya kimaadili mema.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...