Rais
wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua
Bwana Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) nchini.
Taarifa
iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam, leo, Jumatatu, Oktoba 6, 2014, na Kaimu
Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Bwana Peter Ilomo imesema kuwa uteuzi huo umeanza
Ijumaa iliyopita, Oktoba 3, mwaka huu, 2014.
Kabla
ya uteuzi wake, Bwana Mganga alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mkurugenzi
wa Mashitaka na Wakili wa Serikali Mfawidhi.
Imetolewa
na;
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es
Salaam.
6
Oktoba, 2014.
jembe jingine hilo, kazi mnayo mafisadi
ReplyDelete