Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TWTZ) linasikitika kutangaza kifo cha Brigedia Jenerali  (mstaafu) Hashimu Said Mtezo kilichotokea tarehe 04 Oct 14 kwa ugonjwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo     Dar es Salaam alipokuwa akipata matibabu.              
Alizaliwa Machi 18, 1945 Wilaya ya Dodoma mjini katika Mkoa wa Dodoma, alisoma katika shule ya Sekondari ya Tabora kuanzia mwaka 1962 hadi alipohitimu Kidato cha Sita mwaka 1967.  Alijiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania tarehe 20 Juni, 1968.  Alitunukiwa Kamisheni Juni 05,1969.
Katika utumishi wake Jeshini, alihudhuria na kufaulu kozi mbalimbali ndani na nje ya nchi.  Marehemu Brigedia Jenerali Mtezo amewahi kushika madaraka mbalimbali, Mwambata Jeshi nchini Zimbabwe 1987 hadi 1993, Mkurungenzi wa Mafunzo Makao Makuu ya JWTZ 1993 hadi 2002.  Hadi anafariki alikuwa amestaafu Juni 30, 2002 baada ya kulitumikia Jeshi kwa muda wa miaka 34.  Mazishi yatafanyika tarehe 07 Octoba, 2014 Mbezi Lous.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU
BRIGEDIA JENERALI HASHIMU SAIDI MTEZO (MSTAAFU)
AMINA

Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.

Kwa Mawasiliano zaidi: 0783 - 309963

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. RIP Brigadia..michuze mbona hakuna taarifa ya kifo generali muhidin kimario..no aje???????

    ReplyDelete
  2. Rest in Peace Brigadier General Mtezo. Seif, my old classmate, poleni sana na huu msiba mzito. My condolences to the family. K

    ReplyDelete
  3. inna lilah waina ilah rajiun.....hakika ss ni wa mwenyez mungu na kwake tutarejea.....rip brg.general mtezo....pole mariam,jambo,seif n said mtezo....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...