Ajali mbaya imetokea jioni ya leo katika eneo la Tengeru, jijini Arusha ikihusisha gari dogo aina ya Toyota Hiace (pichani juu) linalofanya safari zake kati ya Usa River na Katikati ya mji wa Arusha na Lori la Mafuta. Chanzo cha Ajali hiyo inaelezwa kwamba ni hiyo daladala lilikuwa likijaribu kulipita gari jingine ndipo likakutana na loli hilo la mafuta na kugongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya abiria wote waliokuwa kwenye daladaa hilo ambao idadi yake haijafahamika rasmi. Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Serikali itoe elimu kwa madereva ambao walio chakachua reseni hawana ujuzi wa kudrive, ili waelewe nini maana ya no overtake na kill your speep. Bila ya hivyo ajali zitakua haziishi hapa nchini.

    ReplyDelete
  2. Enough is enough, this is waaaay too much kwa madereva wa tanzania , TERRIBLE COUNTRY

    ReplyDelete
  3. POLENI SANA WAFIWA WA AJALI HII. MUNGU AWAPATIE NGUVU NEEMA NA AMANI WAKATI HUU WA MSIBA.

    ReplyDelete
  4. Ukipoteza mtu unayemfahamu katika ajali hizi ndiyo unaona jinsi ambavyo maisha ya watu yanapotea bure kwa sababu ya haraka au matukio ambayo yangeweza kuzuilika.

    ReplyDelete
  5. Spidi ya fasta fasta itatumaliza!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...