Jumuiya ya wa-Islam wanaozungumza ki-Swahili ktk mji wa
Coventry uliopo nchini Uingereza (United Kingdom), wameadhimisha swala ya Eidil
hajj kwa mafaniko makubwa.
Pamoja na mambo mengine waliandaa sherehe za Eid ambazo
ziliendelea kwa muda wa siku mbili mfulilizo Jumamosi 4/10/2014 na Jumapili 5/10/2014 ambapo vyakula vya kiasili
vitaandaliwa.
Sherehe hizo pamoja na mambo mengine zina malengo ya kuzikusanya pamoja familia kwa
ajili ya kujenga jamii yenye nguvu na yenye kuhimizana maadili mema.
Malengo
hasa ya jumuiya ni kuhakikisha kua jamii inakua pamoja kwani kwa kufanya hivyo
inaamini kwamba itapatikana fursa ya kuwafundisha watoto na watu wazima malezi
bora ikiwa ni pamoja na kuifahamu vizuri dini yao, utamaduni wao na kuhimizana
mambo mema ambayo ulimwengu mzima unahangaika kuhakikisha kwamba, dunia inakua
ni mahali pa amani na utulivu.
Kwa ajili ya kuifahamu
zaidi COMSWA na malengo yake tembelea http://www.comswa.com/
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...