Mwanadada Laveda kutoka Tanzania akilakiwa kwa shangwe alipoingia ndani ya jumba la Big Brother Africa Hotshots usiku wa leo baada ya kushinda kwa kura nyingi sana shindano la vipaji ambapo kila mshiriki alipewa nafasi ya dakika tatu kuonesha kipaji chake. Laveda aliingia na Saxophone na kufurahisha kadamnasi kwa umahiri wake na hatimaye akapewa cheo cha kiongozi wa nyumba wa kwanza katika onesho hili kwa mwaka huu.
Laveda akipuliza saxophone kwa umahiri mkubwa uliompa kura kibao usiku huu. Yaani hapa hata King Maluu atapiga saluti...
Good...............
ReplyDeletemm....mmm ..mmm...lakini.... mbona kama rangi za bangiri alizovaa mkononi huyu anayeitwa mwakilishi wa hii nchi nzuri, ukizitazama kwa makini na kwa ujumla wake unapata taswira ya bendera ya nchi fulani ya EAC?
Naomba nielimishwe vema, maana kuuliza ni moja ya kukuza ufahamu au maarifa.
Mzalendo
Hongera kwa mrembo. Kwakweli mwanzo wake ni mzuri. Kazi iko kwa kaka mwakilishi wetu. Jamani yeye lengo lake kwenda Big Brother ni si lingine ila ni totoz. Yaani yeye hata ushindi hauwazii... kha!
ReplyDelete