Na Magreth Kinabo

WANANCHI   wameshauriwa kuisoma Katiba Mpya Inayopendekezwa  sura kwa sura na ibara kwa ibara ili waweze kupata uelewa wa masuala mbalimbali yaliyomo ndani ya Katiba hiyo na kuacha kusikiliza maneno  ya watu yenye nia ya kupotosha ukweli.

Kauli hiyo ilitolewa jana  na  Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha   Rose Migiro wakati  wa sherehe za mahafali ya pili ya Shule ya Sekondari ya Wasichana  wanaoishi katika mazingira hatarishi  ya WAMA  Nakayama, iliyopo  wilayani Rufiji  mkoani Pwani.

Dkt . Migiro  ambaye  alikuwa mgeni  rasmi katika sherehe hiyo, ambayo ilihudhuriwa na  baadhi ya viongozi , wakiwemo  baadhi ya wake za viongozi   na wageni  wengine mbalimbali.

“Nchi yetu ilikuwa katika mchakato wa uandikaji wa Katiba Inayopendekezwa kazi  ambayo ilikamilika Oktoba 8, mwaka huu. 
 kazi iliyombele  yenu  ni kuisoma Katiba hii sura kwa sura ibara kwa ibara. 

"Tusikubali kusomewa  na tutakapokamilisha kazi ya kuisoma tuipigie kura ya ndiyo,” alisema Dkt. Migiro.

Akizungumza na katika mkutano wa mabalozi wanazoziwakilisha nchi zao katika Jamhuri ya Watu wa China uliofanyika kwenye Nyumba ya kufikia Wageni ya Serikali ya Diaoyutai, Beijing, Rais wa Jakaya Kikwete alisema Kura ya Maoni inatarajiwa  kupigwa wakati wowote Aprili mwaka ujao kama mambo yataenda vizuri.

Rais Kikwete alikabidhiwa Katiba hiyo hivi karibuni mjini Dodoma baada ya Bunge Maalum la Katiba kumalizia kaze yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Wananchi pia wapewe rasimu ya tume ili wajue yaliyoondolewa boreshwa na mapya kabisa ili kubaini ujanja ijanja ama wa tume, bmk, ccm au ukawa ili mwananchi aweze kufanya uamuzi sahihi na si ushabiki wa vyama kama tulivyoshuhudia kwenye bunge la katiba. Tovuti ya tume irudishwe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...