Na Magreth Kinabo
WANANCHI wameshauriwa kuisoma Katiba Mpya Inayopendekezwa sura kwa sura na ibara kwa ibara ili waweze kupata uelewa wa masuala mbalimbali yaliyomo ndani ya Katiba hiyo na kuacha kusikiliza maneno ya watu yenye nia ya kupotosha ukweli.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha Rose Migiro wakati wa sherehe za mahafali ya pili ya Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi katika mazingira hatarishi ya WAMA Nakayama, iliyopo wilayani Rufiji mkoani Pwani.
Dkt . Migiro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo, ambayo ilihudhuriwa na baadhi ya viongozi , wakiwemo baadhi ya wake za viongozi na wageni wengine mbalimbali.
“Nchi yetu ilikuwa katika mchakato wa uandikaji wa Katiba Inayopendekezwa kazi ambayo ilikamilika Oktoba 8, mwaka huu.
kazi iliyombele yenu ni kuisoma Katiba hii sura kwa sura ibara kwa ibara.
"Tusikubali kusomewa na tutakapokamilisha kazi ya kuisoma tuipigie kura ya ndiyo,” alisema Dkt. Migiro.
Akizungumza na katika mkutano wa mabalozi wanazoziwakilisha nchi zao katika Jamhuri ya Watu wa China uliofanyika kwenye Nyumba ya kufikia Wageni ya Serikali ya Diaoyutai, Beijing, Rais wa Jakaya Kikwete alisema Kura ya Maoni inatarajiwa kupigwa wakati wowote Aprili mwaka ujao kama mambo yataenda vizuri.
Rais Kikwete alikabidhiwa Katiba hiyo hivi karibuni mjini Dodoma baada ya Bunge Maalum la Katiba kumalizia kaze yake.
Wananchi pia wapewe rasimu ya tume ili wajue yaliyoondolewa boreshwa na mapya kabisa ili kubaini ujanja ijanja ama wa tume, bmk, ccm au ukawa ili mwananchi aweze kufanya uamuzi sahihi na si ushabiki wa vyama kama tulivyoshuhudia kwenye bunge la katiba. Tovuti ya tume irudishwe.
ReplyDeleteHongera
ReplyDelete