Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi DAVID MISIME  - SACP ameeleza kuwa kutokana na tukio la kihistoria ambalo litafanyika tarehe 08/10/2014 ambapo Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. JAKAYA MRISHO KIKWETE na Mh. Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr. ALLY MOHAMED SHEIN watakabidhiwa Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, ulinzi umeimarishwa katika maeneo yote ya Mkoa wa Dodoma hususani Dodoma Mjini.

Kamanda MISIME amesema ufuatiliaji wa taarifa mbalimbali na kuzifanyia kazi umeimarishwa zaidi, doria za miguu, magari, pikipiki na mbwa na farasi nazo zimeimarishwa. Pia vyombo vyote vya dola tumeimarisha zaidi ushirikiano hasa kubadilishana taarifa mbalimbali na wote mitaani kufuatilia tukio hili muhimu kwa kutumia mbinu zote walizo nazo.

Kamanda MISIME ameendelea kusema niwahakikishie wananchi wa Mkoa wa Dodoma na wageni wote kuwa ulinzi na usalama umeimarishwa tunachowaomba ni ushirikiano wao pale watakapomtilia mashaka mtu yeyote  au jambo lolote wajulishe Polisi haraka nao watalifanyia kazi. Vilevile wenye nyumba za kulala wageni waimarishe ulinzi kwenye maeneo yao ya biashara na kuwapa maelekezo sahihi wafanyakazi wao na wakitilia shaka mgeni yeyote watoe taarifa Polisi.

Aidaha Kamanda MISIME amewataka wananchi wote pamoja na wageni wote watii sheria bila shuruti na yeyote anayepanga kukiuka sheria ili kuvunja amani na utulivu atashurutishwa kwa nguvu zote kwa mujibu wa sheria za nchi na kwa mamlaka waliyopewa  Jeshi la Polisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Habari ndiyo hiyo Ukawa, kazi kwenu safari hii mtazaa na sisi wa Serikali mbili!

    Si mlisusa?,,,Katiba ndiyo hiyoooo inapiga mbawa kuelekea mikononi mwa Raisi!!!

    ReplyDelete
  2. subirienzi kazi yenu.wapigakura si wanainch!!

    ReplyDelete
  3. Tukumbuke yalio tokea Kenya, tupate mafunzo.
    Nilazima tuwe watulivu kila mtu atumie kura yake wakati ukifika hakuna haja ya kufanya uchochezi.

    ReplyDelete
  4. Maandamano mazuru watangulize wake zao na watt zao na wazazi wao wakae mbele hata sisi tutawaunga mkono

    ReplyDelete
  5. Kwani hatuyaoni kazi ohh hatukubali nini mbona hizo pesa wanazofadhiliwa na wathamini wananenepa na family zao hakuna nini wala nini mstari wa mbele uwr ni nafasi ya bb na mm na wake na watoto zao wasituone wajinga

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...