Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi DAVID MISIME - SACP ameeleza kuwa kutokana na tukio la kihistoria ambalo litafanyika tarehe 08/10/2014 ambapo Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. JAKAYA MRISHO KIKWETE na Mh. Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr. ALLY MOHAMED SHEIN watakabidhiwa Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, ulinzi umeimarishwa katika maeneo yote ya Mkoa wa Dodoma hususani Dodoma Mjini.
Kamanda MISIME amesema ufuatiliaji wa taarifa mbalimbali na kuzifanyia kazi umeimarishwa zaidi, doria za miguu, magari, pikipiki na mbwa na farasi nazo zimeimarishwa. Pia vyombo vyote vya dola tumeimarisha zaidi ushirikiano hasa kubadilishana taarifa mbalimbali na wote mitaani kufuatilia tukio hili muhimu kwa kutumia mbinu zote walizo nazo.
Kamanda MISIME ameendelea kusema niwahakikishie wananchi wa Mkoa wa Dodoma na wageni wote kuwa ulinzi na usalama umeimarishwa tunachowaomba ni ushirikiano wao pale watakapomtilia mashaka mtu yeyote au jambo lolote wajulishe Polisi haraka nao watalifanyia kazi. Vilevile wenye nyumba za kulala wageni waimarishe ulinzi kwenye maeneo yao ya biashara na kuwapa maelekezo sahihi wafanyakazi wao na wakitilia shaka mgeni yeyote watoe taarifa Polisi.
Aidaha Kamanda MISIME amewataka wananchi wote pamoja na wageni wote watii sheria bila shuruti na yeyote anayepanga kukiuka sheria ili kuvunja amani na utulivu atashurutishwa kwa nguvu zote kwa mujibu wa sheria za nchi na kwa mamlaka waliyopewa Jeshi la Polisi.
Habari ndiyo hiyo Ukawa, kazi kwenu safari hii mtazaa na sisi wa Serikali mbili!
ReplyDeleteSi mlisusa?,,,Katiba ndiyo hiyoooo inapiga mbawa kuelekea mikononi mwa Raisi!!!
subirienzi kazi yenu.wapigakura si wanainch!!
ReplyDeleteTukumbuke yalio tokea Kenya, tupate mafunzo.
ReplyDeleteNilazima tuwe watulivu kila mtu atumie kura yake wakati ukifika hakuna haja ya kufanya uchochezi.
Maandamano mazuru watangulize wake zao na watt zao na wazazi wao wakae mbele hata sisi tutawaunga mkono
ReplyDeleteKwani hatuyaoni kazi ohh hatukubali nini mbona hizo pesa wanazofadhiliwa na wathamini wananenepa na family zao hakuna nini wala nini mstari wa mbele uwr ni nafasi ya bb na mm na wake na watoto zao wasituone wajinga
ReplyDelete