Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu
za rambirambi Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt.
Hussein Mwinyi, kuomboleza kifo cha Meja Jenerali Muhidin Kimario, Waziri Mwandamizi
wa Zamani wa Serikali na Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (TPDF).
Aidha,
Rais Kikwete amewatumia pole nyingi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali
Davis Mwamunyange na familia ya Meja Jenerali Kimario kufuatia kifo hicho
kilichotokea mchana wa leo, Jumatatu, Oktoba 6, 2014, nchini India, ambako
alikuwa anapata matibabu.
Amesema
Rais Kikwete katika salamu hizo kwa Waziri Mwinyi: “Nimepokea kwa masikitiko makubwa
taarifa za kifo cha Meja Jenerali Muhidin Kimario, ambaye alilitumikia Jeshi
letu kwa heshima kubwa na weledi wa kuigwa na baadaye kulitumikia Taifa letu
kwa uaminifu na uadilifu wa kujivunia katika nafasi ya uwaziri.”
Ameongeza
Rais Kikwete katika rambirambi zake: “Uhodari na ujasiri ule ule ambao Meja Jenerali
Kimario aliuonyesha akiwa askari na ofisa mkuu ndio ule ule uliomwongoza katika
utumishi wa umma na kwa nafasi zote za waziri mwandamizi, ambazo alizishikilia katika
maisha yake iwe ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Waziri wa Mambo
ya ndani ya Nchi, Mkuu wa Mkoa ama Mkurugenzi wa Ustawishaji wa Makao Makuu
(CDA). Daima tutakosa uongozi na ushauri wake.”
“Nakutumia
wewe Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa salamu za dhati ya moyo wangu
kuomboleza kifo hiki. Aidha, kupitia kwako, namtumia pole nyingi Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na Jeshi letu lote kwa kuondokewa
na ofisa mwenzao, kiongozi wao na mpiganaji mwenzao,”
amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Aidha,
kupitia kwako, natuma salamu zenye huzuni nyingi kwa familia ya Meja Jenerali
Muhidin Kimario. Wajulishe kuwa niko nao katika msiba huu mkubwa wa kuondokewa
na mhimili wa familia. Vile vile wajulishe kuwa naungana nao katika kumwomba
Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke peponi roho ya Marehemu. Amin.”
.jpg)
Dkt.
Shija aliyefariki dunia Jumamosi asubuhi mjini London, Uingereza, ambacho
ndicho kilikuwa kituo chake cha kazi, alisomea na kuwa mhadhiri wa uandishi wa
habari kabla ya kuwa mbunge wa Sengerema kwa miaka 15 mfululizo na Waziri
Mwandamizi wa Serikali katika Wizara mbali mbali.
Katika
salamu zake kwa Sekretarieti ya CPA, Kanda ya Afrika, Rais Kikwete amesema kuwa
amestushwa sana na kifo cha Dkt. Shija ambacho kimeinyang’anya Afrika na dunia,
na hasa Tanzania na Jumuia ya Madola, mtumishi mwadilifu na mwaminifu, ambaye
alitoa maisha yake kwa utumishi wa umma.
“Alikuwa
kiongozi mfano katika nafasi zote za umma alizozishikilia. Aliifanya kazi yake
ya uhadhiri wa uandishi wa habari kwa ufanisi mkubwa na aliwapa utumishi
uliotukuka wananchi wake wa Sengerema katika nafasi yake ya Ubunge. Dkt. Shija
alitumainiwa sana katika nafasi zote nyingi na za uandamizi za Uwaziri wa
serikali,” amesema rais Kikwete na
kuongeza:
“Nawatumieni
salamu za dhati ya moyo wangu kuomboleza kifo cha Dkt. Shija na naungana nanyi
katika kumlilia. Kupitia kwenu, nawatumia wajumbe wote wa CPA na Sekretarieti
ya Chama hicho pole nyingi sana kwa kuondokewa na kiongozi na mtendaji wao
mkuu. Aidha, naomba pia mniwasilishie pole zangu kwa wana-Sengerema ambao Dkt.
Shija aliwatumikia kwa uaminifu na kwa miaka mingi.”
“Wajulisheni
wote kuwa niko nao katika msiba huu mkubwa na naomboleza nao na niko nao katika
kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweka peponi roho ya Marehemu
William Shija. Amin.”
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
– Dar es Salaam.
6 Oktoba, 2014.
Inallilah wa inna ilayhi rajiun,
ReplyDeleteLala pema Mzee wetu Mzee Kimario.