Zoezi Ushirikiano imara limefunguliwa leo hii nchini Burundi katika mkoa
wa Mwaro, Mgeni rasmi katika ufunguzi huo alikuwa Makamu wa kwanza
wa Rais wa Burundi mhe.Prosper Bazombanza.
Katika ufunguzi huo mhe
Bazombanza amesema kuwa ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika
mashariki umetokana na makubaliano ya wakuu wa nchi wanachama
yaliyofanyika mwaka 2001,hivyo kuzitaka nchi shiriki kuenzi makubaliano
hayo kwa kushiriki mara kwa mara katika mazoezi hayo.
Amesema ushiriki katika mazoezi haya unajenga kujiamini kwa majeshi
ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuwafanya wanajeshi wa Jumuiya
hii kutambua kuwa wapo pamoja katika masuala ya ulinzi. Gwaride rasmi
lilipita mbele ya mgeni rasmi kwa heshma huku Wakuu wa Majeshi na
wawakilishi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakihudhuria sherehe
hizo.
Kwa upande wa Tanzania sherehe hizo zimehudhuriwa na Mkuu wa
mafunzo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Meja Jenerali James
Mwakibola pamoja na mwambata wa JWTZ nchini Burundi kanali Venant
Mutashobya ambaye kabla ya ufunguzi wa zoezi hili wakati wote alikuwa
akivipokea vikundi kutoka Tanzania akianzia kupokea kikundi cha JWTZ
kilichokwenda Burundi kwa njia ya barabara katika mpaka wa kabanga
na baadaye kupokea kikundi cha wanamaji wa JWTZ kupitia mpaka wa
Kagunga.
Zoezi ushirikiano imara ni moja ya mazoezi muhimu
yanayolifanya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania kuendelea
kuwa moja ya majeshi yenye weledi wa hali ya juu katika
kutekeleza majukumu yake kitaifa na kimataifa. Zoezi hilo
linafanyika nchini Burundi kuanzia tarehe 13 hadi 26 Oct 2014
ambapo hushirikisha majeshi ya nchi za jumuiya ya afrika
mashariki za Burundi,Kenya,Rwanda,Tanzania na Uganda.
Mazoezi ya pamoja kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yameendelea
kufanya majeshi katika ukanda huu kuwa na weledi kiutendaji hii ni
kutokana na majeshi haya kubadilishana uzoefu katika Nyanja za kiulinzi
na usalama.
Wakati huohuo Tanzania imeteuliwa kuongoza zoezi hilo huku Brigedia
Jenerali Joseph Cosmas Chengelela kuchukuwa jukumu la kuongoza
kombaini ya vikundi vitakavyo shiriki zoezi hilo.
Akiongea mara baada
ya ufunguzi, Mkuu wa zoezi kutoka Tanzanina Brigedia Jenerali Joseph
Chengelela amesema ushiriki wa JWTZ katika mazoezi haya unalifanya
JWTZ kuwa miongoni mwa majeshi bora katika ukanda huu kwani ni njia
moja wapo ya kuwafanya maafisa na askari kujifunza mambo mbalimbali
kutoka kwa majeshi mengine ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Brigedia Jenerali Joseph Chengelela (kushoto)akimkabidhi bendera ya Afrika Mashariki msaidizi wa
zoezi mara baada ya kukabidhiwa kutoka kwa mgeni rasmi hayupo pichani siku ya ufunguzi wa zoezi
USHIRIKIANO IMARA 2014-BURUNDI.
Meja Jenerali James Mwakibolwa wa nne kulia akiwa na Brigedia Jenerali Joseph Chengelela wa tano
kulia na Mwambata wa JWTZ nchini Burundi kanali Venant Mutashobya wa tatu kulia mara baada ya
ufunguzi wa zoezi USHIRIKIANO IMARA 2014-BURUNDI.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...