Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto)
akizungumza na wajumbe wa Baraza Dogo la Wafanyakazi la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
kabla ya kulizindua Baraza hilo katika Hoteli ya Livingstone mjini Bagamoyo leo. Katika
hotuba yake, Abdulwakil aliwataka viongozi wakuu wa jeshi hilo kushirikiana kikamilifu na
watumishi wote ili kuleta mabadiliko chanya ndani ya jeshi hilo. Wapili kulia ni Kamishna
Jenerali wa Jeshi hilo, Pius Nyambacha, Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa
Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Zimamoto na Uokoaji, Shwaybu Mohamoud. Watatu
kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Tume ya Usuluhishi na Upatanishi (CMA), Andrew Mwalisisi
na wapili kushoto ni Katibu wa Tughe tawi hilo, Andason Kalewa.
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha (kushoto) akitoa
hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mbarak Abdulwakil (wapili kulia-meza kuu) kuzungumza na kulizindua Baraza Dogo la
Wafanyakazi la Jeshi hilo. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na
Afya (Tughe) tawi la Zimamoto na Uokoaji, Shwaybu Mohamoud. Watatu kulia ni Mkurugenzi
Msaidizi wa Tume ya Usuluhishi na Upatanishi (CMA), Andrew Mwalisisi na wapili kushoto ni
Katibu wa Tughe tawi hilo, Andason Kalewa. Uzinduzi wa Baraza hilo ulifanyika katika Hoteli
ya Livingstone mjini Bagamoyo leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (watano kushoto-
waliokaa), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa (watano
kulia), Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali, Pius Nyambacha (wanne
kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza Dogo la Wafanyakazi wa Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji baada ya kuzinduliwa baraza hilo katika Hoteli ya Livingstone mjini
Bagamoyo leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...