Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsifia Mbunge wa Jimbo la Isimani, William Lukuvi kwa uchapakazi wake mzuri wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Magozi, Kata ya Ilolo Mpya, Iringa Vijini leo. Kinana alimjia juu Waziri wa Maliasili na Utalii, Nyalandu kwa kushindwa kutafutia ufumbuzi migogoro ya wananchi.Pia aliwataka wananchi kuacha kukwepa majukumu yao ya kuwatumikia Wananchi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye akihutubia katika mkutano huo
Kinana akisalimiana na wananchi alipowasili kushiriki ujenzi wa jengo la CCM tawi la Luganga Kata ya Ilolo Mpya.
Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana na Mbunge wa Jimbo la Isimani, William Lukuvi wakishiriki kufyatua tofali za ujenzi wa jengo la Ofisi ya CC,
Kinana na Lukuvi wakisaidia kufyatua tofali za kujengea jengo hilo la CCM.
Wau wengine mikoa tunaiangalia kwenye picha hizi tukiangalia tunajiuliza sasa hapa ndio mjini yaani central business district ya mkoa au ni pembeni?
ReplyDelete