Mfuko
wa Maendeleo ya Jamii TASAF umeanza hatua ya kutambua kaya maskini
katika mikoa ya Mwanza,Shinyanga,Tanga, Morogoro,Pwani na Simiyu ikiwa
ni utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini PSSN unaoratibiwa na
mfuko huo nchini kote kwa awamu. Akifungua warsha ya kuwajengea uelewa
viongozi wa wilaya ya Maswa ,Mkuu wa wilaya hiyo Luteni Mstaafu Abdallah
Kihato ametoa wito kwa wananchi kuzingatia miongozo ya TASAF ili waweze
kunufaika na mpango huo.
Amesema serikali wilayani humo itatoa
ushirikiano kwa wataalamu wa TASAF na watendaji wengine ili zoezi la
kuzibaini kaya maskini liweze kufanikiwa. Kwa upande wake meneja fedha
wa TASAF Bw. Njego Nyamukowa kwa niaba ya mkurugenzi Mtendaji wa TASAF
Bwana Ladislaus Mwamanga amesema utekelezaji wa mpango huo unafanyika
kwa mafanikio makubwa .
Mtaalam
kutoka TASAF Bw. Hamis Kikweppe akitoa maelezo juu ya Mpango wa
kunusuru kaya maskini wakati wa warsha ya kujenga uelewa kwa timu ya
wawezeshajio wa wilaya ya Maswa mkoani Simiyu. (2)
Meneja
wa Fedha wa TASAF Bw.Njego Nyamuko aliyeshika kipaza sauti mbele akitoa
maelezo juu ya Mpango wa kunusuru kaya maskini unaoendeshwa na TASAF
katika warsha ya kuwajengea uelewa viongozi wa wilaya ya Maswa.
Mkuu wa wilaya ya Maswa Luteni Mstaafu Abdallah Kihato akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya kujengewa uwezo juu ya mpango wa kunusuru kaya maskini katika wilaya ya Maswa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...